Mwana
mitindo wa rap Martin Bambara, almaarufu Smockey, ni kiongozi wa shirika
la kiraia la Balai citoyen, hapa ni kwenye eneo la Taifa katika mji wa
Ouagadougou, Septemba 16, 2015.
Na RFI
Jenerali
Gilbert Diendéré, mkuu wa kikosi cha ulinzi wa (RSP), ameipindua
serikali na kuchukua uongozi wa nchi ya Burkina Faso. Lakini mashirika
ya kiraia na vyama vya siasa vimeapa kutokubali mapinduzi hayo ya
kijeshi. Katika nchi nzima, mashirika ya kiraia na upinzani wamesimama,
hasa katika vijana ili kutokubaliana na mapinduzi hayo ya kijeshi.
Chini ya
mwaka mmoja baada ya maandamano yaliyomnga'tua madarakani Blaise
Compaoré, na wakati ambapo demokrasia nchini Burkina Faso imekua
ikionekana ikianza kujidhatiti, zikisalia siku chache kabla ya uchaguzi
wa rais na wabunge Oktoba 11, mapinduzi ya kijeshi yanauweka hatarini
mchakato huo.
Tangu
Jumatano usiku wiki hii, raia wa Burkina Faso waliingia mitaani ili
kuonyesha ghadhabu zao dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa na
kikosi cha ulinzi wa Rais (RSP). Tangu mapinduzi ya kijeshi kutangazwa,
mashirika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na shirika la Balai Citoyen,
yamekua yakitolea wito raia wa Burkina Faso na jeshi kutetea demokrasia
yao. Katika mikoa, wito umeitikiwa, hasa kwa vijana wa Burkina Faso.
Nchini kote, vijana ndiowameonekana mitaani Alhamisi wiki hii,
wameandamana pamoja na mashirika ya haki za binadamu , na vyama vya
mbalimbali vya wafanyakazi.
Katika
mji wa Bobo Dioulasso, mji wa pili nchini humo, raia wameandamana bila
hata hivyo kusubiri tangazo la mapinduzi ya serikali. IWaandamanaji hao
wamekua wakisema: "mumuachiliye huru Zida" " mumuachiliye huru Kafando".
Arsène Kamsie ni kiongozi wa harakati za vijana katika mji wa Bobo
Dioulasso amesema: "tumeanza kujianda ili kupinga mapinduzi haya, kwa
sababutunahisi kwamba wametusaliti. "
Nyumba ya Dienbéré yachomwa kwa moto
Hakuna
maduka yaliofunguliwa vivyo hivyo katika mkoa wa Ouahigouya,
Kaskazini-Magharibi na katika mkoa wa Tenkodogo, katikati mwa nchi. Kila
mahali, shughuli mbalimbali zimekwama katika miji tofauti: kama katika
mji wa Banfora, karibu na mpaka na Côte d'Ivoire: wakaazi wameweka
vizuizi barabarani.
Katika
mji wa Yako alikozaliwa jenerali Gilbert Diendéré, nyumba kadhaa
zimechomwa, ikiwa ni pamoja na nyumba ya mkuu huyo wa kikosi cha ulinzi
wa Rais aliyeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi.
No comments:
Post a Comment