Dar es Salaam.
Tofauti na wasanii wengine ambao tayari wamejipambanua kisiasa, mwimbaji wa r&b nchini Ben Pol ana fikra tofauti na wenzake wengi, baada ya kuweka wazi kilichoujaza moyo wake kuhusu siasa.
Tofauti na wasanii wengine ambao tayari wamejipambanua kisiasa, mwimbaji wa r&b nchini Ben Pol ana fikra tofauti na wenzake wengi, baada ya kuweka wazi kilichoujaza moyo wake kuhusu siasa.
Ben Pol anayetamba na wimbo
“Sophia” amesema wakati wasanii wengine wakijivika magwanda ya vyama,
yeye amejiweka pembeni akitafakari, kwani anahisi hafai kufuata mkumbo
ila moyo wake unaamua nini kwa mustakabali wa taifa lake.
Akizungumza
na Mwananchi jana, Ben Pol aliweka wazi kwamba kinachoendelea katika
kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa sasa kinamfanya afikirie zaidi ya mara
mbili, iwapo wasanii wenzake na vijana wanaotumika kisiasa kama wanajua
wanachokifanya na iwapo wamesoma kwa uhakika ilani za vyama
wanavyoshabikia.
Alisema kubwa kwake ni sera za
wagombea huku amani na utulivu wa nchi ni vitu anavyoomba usiku na
mchana viendelee hata baada ya Oktoba 25.
“Kura yangu
ina thamani kubwa, mashabiki wengi pia wananiuliza kwanini siweki
chochote katika kurasa zangu za mitandao ya kijamii au kujumuika na
wengine katika kampeni, mimi ni msanii na mfanyabiashara siwezi
kuchanganya mambo. Lakini kubwa zaidi bado nafikiria nani nimpe kura
yangu na naendelea kufuatilia ilani za vyama na vipaumbele vyao ili
nijue nafanya nini Oktoba 25,” alisema Ben Pol.
Alisisitiza
kuwa vijana wanatakiwa kutulia na kutafakari kwa makini, kabla
hawajaamua kupiga kura na watakayemchagua atafanya nini na nini.
“Vijana
wengi wanatumika, msikilize mgombea sera zake na tafakari kwa kina na
namna atakavyoweza kuzitekeleza, ukiridhika kampigie kura,” alisema Ben
Pol
No comments:
Post a Comment