Rais
wa Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa, Bw. Sam Kutesa akigonga nyundo
maalum kuashiria kukamilika kwa Mikutano ya Baraza hilo ambalo
ameliongoza kwa mwaka mzima. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki Moon akiwa mwenye furaha wakati wa kuhitimishwa Baraza
la 69 ambapo alimpongeza Bw. Sam Kutesa kwa kuliongoza Baraza kwa
uhodari uliopelekea kupitishwa kwa maazimio mbalimbali.
Na MwandishiMaaalum New
York
Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,
uliokuwa chini ya Urais wa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uganda Bw, Sam Kutesa umefikia ukingoni siku ya jumatatu
kwa kupitisha maamuzi ya kihistoria ambayo pamoja na
mambo mengine yanatoa mwelekeo wa majadiliano kuhusu
marekebisho na mageuzi ya Baraza Kuu
la Usalama la Umoja
wa Mataifa.
Maamuzi hayo ambayo kwa mara ya
kwanza yanaingizwa
rasmi katika nyaraka muhimu za Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa na yaliyopewa namba
A/69/L.92 yalipitishwa kwa
kauli moja na wajumbe kutoka nchi 193 wanaounda Baraza
Kuu la
Umoja wa Mataifa.
Maamuzi hayo ambayo baadhi ya wazungumzaji
waliyapachika jina kama maamuzi ya Kutesa ikiwa ni ishara
ya kutambua mchango
wake katika kusimamia kidete
majadiliano kuhusu mageuzi ya Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa yanatoa msingi au
maandishi ambayo
yatawawezesha Nchi Wanachama kujadiliana kwa kupitia
maamuzi hayo.
Ingawa maamuzi hayo yamepita bila kupigiwa kura na
kupongezwa kwa kufungua ukursa mpya katika kuendeleza
mchakato wa majadiliano ya mageuzi na upanuzi wa Baraza
Kuu
la Usalama, baadhi ya nchi zimeyaelezea maamuzi hayo
kuwa ni ya kiufundi zaidi na hivyo yasikuchukuliwe kama
maamuzi ya mwisho kwa madai kwamba, maandalizi na
majadiliano ya maamuzi hiyo hayakuwajumuisha na hivyo
hayawakilishi nina hisia za makundi yote.
Akiungana na wazungumzaji wengi waliounga mkono
kupitishwa kwa maamuzi hayo Mwakilishi wa Kudumu wa
Akasema hapana shaka kwamba majadiliano Zaidi
yanapaswa kuendelea ili kujibu kiu ya kila upande na
kwamba nchi wanachama wanapaswa kujivunia hatua
hiyo muhimu hata kama ni hatua ndogo.
Akatumia fursa hiyo kuwapongeza Bw.Sam Kutesa na
Mwakilishi wa kudumu wa
Jamaica Balozi Rattray kwa kazi
nzuri , kubwa na iliyokuwa na changamoto nyingi lakini
iliyofanikisha kupatika kwa maamuzi hiyo.
Majadiliano kuhusu namna ya kuboresha na kupanua
wigo wa wajumbe wa Baraza Kuu
la Usalama la Umoja
wa Mataifa,
ni majadiliano yaliyoaza mwaka 2008 lakini
ni katika Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la
Umoja wa
Mataifa ambapo matokeo ya majadiliano miongoni mwa
wanachama yameweza kupitishwa rasmi katika Baraza
Kuu
la Umoja wa Mataifa.
Muundo wa sasa wa Baraza Kuu la Usalama la
Umoja
wa Mataifa ambalo lina wajumbe wakudumu na wenye
kura ya turufu watanona wajumbe 10
wanaoingia kwa
mzunguko wa uwakilishi wakiandaa haujaitendea haki
Afrika bara ambalo lilokumbwa kwa asilimia kubwa ya
maamuzi yanayofanywa na Baraza Kuu
la Usalama
yanaihusu Afrika lakini Afrika si mwanachama wa
kudumu na hiyvo imekuwa ikipigania kupata nafasi ya
uwakilishi wa kudumu pamoja na kura ya turufu.
Kumalizika kwa Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu
la
Umoja wa Mataifa, kunafungua kuanza kwa Mkutano
wa Baraza Kuu la 70
ambalo kwa mwaka mzima
litakuwa chini ya Urais wa Bw.Monges Lykketoft.
No comments:
Post a Comment