Mgombea ubunge wa jimbo la Lushoto, mkoani Tanga kwa tiketi
ya Chadema, Mohamed Mtoi amefariki baada ya gari lake kupinduka wakati
akitokea kwenye kampeni.
Akithibitisha taarifa hizo
zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, Katibu wa Chadema
wilayani Lushoto, Abdalah Dhahabu amesema ajali hiyo imetokea jana jioni
wakati mgombea huyo akitokea Mlola alipokuwa anafanya kampeni kuwania
kiti hicho.
“Ni kweli Mtoi ametutoka na hapa nipo
nyumbani kwa marehemu Mkunzi. Hapa (jana usiku) tunangojea taarifa za
wanandugu tujue taratibu za maziko,” amesema katibu huyo.
Akieleza
namna ajali ilivyotokea, Dhahabu amesema wakati Mtoi alipomaliza
mkutano wake wa kampeni Mlola, alipanda gari kurudi nyumbani kwake eneo
la Mkunzi ndipo lilipoacha njia na kupinduka na mwanasiasa huyo kufariki
papo hapo.
Akizungumzia hali ya dereva wake, katibu
huyo amesema alikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Lushoto na kwamba
afya yake ilikuwa inaendelea vema
No comments:
Post a Comment