Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi
kijana Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa mashine ya kubangulia korosho
vikiwemo meza, vifaa mbalimbali na pikipiki mpya, kupitia mpango wa
Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu
yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe,
Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara,
Bartholomew Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa
Airtel, Happy John (wa tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa
Airtel, Dangio Kaniki.…
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi kijana
Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa mashine ya kubangulia korosho vikiwemo
meza, vifaa mbalimbali na pikipiki mpya, kupitia mpango wa Airtel
‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu yake ya
biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya
Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew
Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy
John (wa tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio
Kaniki.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi kijana
Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa vifaa mbalimbali vya kubangulia
korosho na pikipiki mpya, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara
iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya Mtwara
jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa
pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy John (wa
tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi kijana
Iddy Abdallah Chilumba, msaada wa pikipiki mpya vikiwemo vifaa
mbalimbali vya kubangulia korosho, kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa
Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu yake ya biashara
iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa wa Relwe, Manispaa ya Mtwara
jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel Mtwara, Bartholomew Masatu (wa
pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Happy John (wa
tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Meneja
wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (kulia), akimkabidhi kijana
Iddy Abdallah Chilumba, kadi ya pikipiki mpya iliyotolewa msaada kwake
vikiwemo vifaa mbalimbali vya kubangulia korosho, kupitia mpango wa
Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika kwenye sehemu
yake ya biashara iliyokarabatiwa na Airtel katika Mtaa
wa Relwe, Manispaa ya Mtwara jana. Wanaoshuhudia ni Meneja wa Airtel
Mtwara, Bartholomew Masatu (wa pili kushoto), Meneja wa Huduma kwa
Wateja wa Airtel, Happy John (wa tatu kushoto) na Afisa Uhusiano na
Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki.
Airtel Fursa Yaendela Kuinua Vijana hapa
Nchini Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imemuwezesha mjasiriamali
Idd Chillumba vifaa vya kufanikisha shughuli zake za kufungasha
Korosho ikiwa ni pamoja na usafiri wa kuwezesha kusambaza bidhaa zake
kwa wateja wake kupitia mpango wake wa Airtel Fursa ambapo
vitamuwezesha kuinua maisha yake na familia yake.
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma
kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi amesema, vifaa hivyo vitamuwezesha
Bw. Chillumba kuendeleza biashara yake ya kufungasha Korosho na
kusambaza kwa uharaka zaidi kwa wateja wake. Bi Bayumi amesema, mpango
huo wa kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni
hiyo wa kuwawezesha vijana wenye malengo mazuri na maisha yao, tabia
nzuri, na wenye dhamira ya kujikomboa kimaisha na kuwa wafanyabiashara
wakubwa hapo baadae.
“Sisi kama kampuni ya mawasiliano tumeona
ni vizuri kushirikiana na vijana ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza
mitaji yao ya biashara na kuweza kujiinua kiuchumi, kuweza kufikia
ndoto zao na vile vile kuongeza ajira kwa vijana hapa nchini” alisema
meneja huyo. “Vifaa hivi vitamuwezesha bw.
Chillumba kuongeza biashara yake na kupanua
wigo wa kutoa huduma kwa wateja wake na usafiri huu wa pikipiki utampa
nafuu ya kusafirishia bidhaa zake kutoka sehemu moja kwenda nyingine.”
aliongeza Bi Bayumi Akipokea msaada huo Bw. Chillumba ameshukuru kwa
vifaa na usafiri huo na kuahidi kuendeleza zaidi biashara hiyo ili
kutimiza ndoto zake za kuwa mfanyabiashara mkubwa.
“Sikuamini kama siku moja ningeweza
kufikia malengo yangu katika biashra hii. Mimi ni mtoto wa kwanza katika
familia yetu. Nilizaliwa miaka ishirini na nne iliyopita. Baba yangu
alifariki nikiwa na umri wa mwaka mmoja. Mama yangu hakuwa na uwezo wa
kunifikisha mbali kielimu hivyo niliishia kidato cha nne.
Ilinilazimu kuanza maisha mapema kwa
kuanzisha biashara ya kubangua korosho, fedha ninayopata japokuwa ni
kidogo naitumia kujikimu mimi mwenyewe, kumsaidia mama yangu na ndugu
zangu. Kutokana na msaada huu kutoka Airtel, naahidi kuongeza juhudi na
kutumia vyema msaada huu ili kuhakikisha nakuza na kuendeleza biashara
yangu na kuinua vijana wenzangu hapo baadae”
alisema Chillumba.Kampuni ya simu ya Airtel
inazunguka nchi nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya
ujasiriamali na asha kutoa uwezeshaji kwa vijana ili waweze kukuza
mitaji yao.
No comments:
Post a Comment