Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi wakati akipokea msaada huo kutoka WHO. Kulia ni Mwakilishi wa
Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora.
Taarifa ikitolewa kabla ya kupokea msaada huo.
Hapa wakitiliana saini mkataba wa kupokea msaada huo.
Mwakilishi
wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora (katikati),
akimkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan
Mmbando (kushoto), dawa ya maji zenye thamani ya sh.milioni 42.2
zilizotolewa na WHO kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko nchini, Dar es Salaam leo asubuhi. Anayeshuhudia tukio hilo
kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Uhakiki na Ubora wa Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii, Dk.Mohamed Ali Mohamed.
SERIKALI
imepokea msaada wa dawa ya kutakasa maji ya Waterguard kutoka Shirika
la Afya Duniani (WHO),kwa lengo la kukabiliana na magonjwa ya mlipuko
zenye thamani ya sh. milioni 42.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi mara baada ya kupokea dawa hiyo, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando, alisema dawa
hizo ni waterguard cotton (1000) na Cresol Saponated Liquid (100) litres
ambayo itasaidia kutakasa maji ili kuepusha magonjwa ya mlipuko kama
kipindupindu.
Alisema
dawa hiyo itasaidia kudhibiti ugonjwa huo kwani kila siku zinavyozidi
kwenda wagonjwa wanazidi kuongezeka hivyo dawa hiyo itatumika kupunguza
maambukizi mapya.
"Hali ya
mazingira bado hairidhishi idadi ya wagonjwa inazidi kuongezeka hadi
sasa, tangu ugonjwa uanze kuripotiwa wagonjwa walioripotiwa kwa Dar es
salaam ni 385 na vifo vya watu 8," alisema.
Alitaja
mgawanyiko wa wagonjwa katika kila manispaa Kinondoni 292 , Ilala 60
na Temeke 33, aliongeza idadi ya wagonjwa waliopo kwenye kambi za
matibabu hadi Agosti 27, jumla ni 74 ambapo kituo cha Mburahati 53 ,
Buguruni ikiwa na wagonjwa 14 huku Temeke 7.
"Kwa Mkoa
wa Morogoro idadi ya wagonjwa hadi Agosti 28, wagonjwa 60 na walioko
kambini ni 9 na kifo 1...moja ya sababu ambazo zinachangia kuendelea kua
na ugonjwa huu hapa nchini ni kunywa maji yasiyo safi na
salama,"alisema.
Mmbando
alitoa tahadhali kwa wananchi kujizuia kunywa maji yasiyo safi na
salama,kuepuka kula chakula kilichopoa au kuandaliwa katika mazingira
yasiyo safi hali hiyo itasaidia kutokomeza ugonjwa huo na kuwataka
kuchemsha maji ya kunywa na kuweka dawa.
Akikabidhi
msaada huo Mwakilishi Shirika la afya duniani (WHO), Dr. Rufaro
Chatora alisema anamini dawa hizo zitasaidia kukabiliana na mlipuko wa
ugonjwa wa kipindupindu.
"Msaada
huu tuliyotoa utasaidia wananchi kwa kiasi kikubwa katika kupunguza
maambukizo mapya ya ugonjwa huu ambao huwa unaua kwa kiasi
kikubwa,"alisema.
No comments:
Post a Comment