Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia (kushoto),
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa taarifa ya MSD ya mwaka 2013/2014
uliofanyika Ofisi za MSD Keko jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Kaimu
Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Johnson Mwakalitolo, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia, akizungumza katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Tehama wa MSD, Issaya Mzolo, akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo.
Ofisa
Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye
uzinduzi huo. Kulia ni Meneja wa Uhasibu wa MSD, Sako Mwakalobo.
Keki ya Birthday ya Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani katika muonekano.
Kaimu
Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto), akikata keki hiyo
aliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake wakati wakimpongeza kutimiza miaka
55 ya kuzaliwa kwake. Kulia ni Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi wa MSD,
Doreen Josia. Wafanyakazi hao waliamua kumpongeza Mwaifwani baada ya
kumalizika kwa uzinduzi wa ripoti hiyo.
Mwaifwani akimlisha keki, Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry.
Hapa ni zamu ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD, Profesa Idris Ali Mtulia akilishwa keki.
Mkurugenzi
wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja wa MSD, Edward Terry,
akimlisha keki, Kaimu Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani.
Hapa Katibu Muhtasi wa Mkurugenzi MSD, Dinah Dileya (kushoto), akilshwa keki.
Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamin Massangya (kulia), akigawa ripoti hiyo kwa wafanyakazi wa MSD.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka (kushoto), akizingumza kwenye uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa MSD, wakifuatilia uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa MSD, wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ni furaha
tupu katika uzinduzi huo na hafla ya wafanyakazi hao kumpongeza Kaimu
Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani kutimiza miaka 55 tangu azaliwe.
Viongozi wa MSD wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Hii ni timu ya wajumbe walioandaa ripoti hiyo ya mwaka 2013/2014. 'Big Up wajumbe kwa kazi nzuri'
BOHARI
ya Dawa (MSD) imezindua rasmi taarifa yake ya mwaka 2013/2014 (Annual
Report), ambayo ilizinduliwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Bodi ya
Wadhamini wa MSD, Profesa Idris Ali Mtulia.
Akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo, Profesa Mtulia alisema
kupanda kwa huduma za usambazaji dawa, upatikanaji wa dawa kutoka
asilimia 55 hadi 85 ni jambo la kujivunia.
Kaimu
Mkurugenzi wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema mpango wa MSD kwa sasa ni
kuanzisha maduka ya dawa ambayo yataendeshwa na MSD ambapo kwa kuanzia
hivi karibuni litazinduliwa mkoani Mbeya na baadae itafuatia mikoa Kanda
za Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.
No comments:
Post a Comment