Msanii maarufu wa filamu
nchini, Wema Sepetu, amedai kuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki,
Tundu Lissu wa CHADEMA, siku zake za ubunge zinahesabika kutoka na
kampeni atayosaidiana na mgombea wa CCM wa jimbo hilo Jonathan Njau,
ambayo itaiondoa CHADEMA na kulirejesha jimbo hilo CCM. Wema aliyasema
hayo wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye viwanja vya ofisi ya
CCM wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
MSANII
maarufu wa filamu nchini,Wema Sepetu, amemtangazia kiama mbunge wa
jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu wa CHADEMA,kwamba siku zake za
ubunge zinahesabika.
Wema
miss Tanzania 2006, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa
habari juu ya safari yake ya kisiasa ambayo ameianzisha baada ya
kushindwa kwenye uchaguzi ubunge viti maalum (CCM) mkoa wa Singida
uliofanyika hivi karibuni.
Alisema
matunda ya safari yake ya kisiasa yataanza kuonekana kuanzi oktoba
mwaka huu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, kwani jimbo la Singida
mashariki,litakuwa mikononi mwa CCM chama tawala.
“Mimi
nimerudi Singida kwa kazi maalum, nimekuja kushiriki upigaji kura za
maoni CCM.Tumemchagua mgombea wetu Jonathan Njau…..tutahakikisha Njau
anamgaragara Tundu Lissu”,alisema Wema kwa kujiamini.
Akifafanua,alisema hivi sasa maandalizi ya kuing’oa CHADEMA jimbo la Singida mashariki,yameanza na yanaendelea vizuri.
Wema
alisema kazi ya kuing’oa CHADEMA mwaka huu, itafanywa kwa ushirikiano
wa karibu na wana CCM wote na kuungwa mkono na kundi la wasanii maarufu
kutoka jijini Dar-es-salaam.
Kwa
upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Segamba,amesema Wema
ameonyesha amekomaa kisiasa kwa kitendo chake cha kurudi Singida
mapema,licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa ubunge viti maalum CCM
hivi karibuni.
“Tunaendeleaa
kushuhudia wana CCM wengi wanaoangushwa kwenye chaguzi mbalimbali,huwa
na chuki na chama na wangine wamefikia uamuzi wa kukihama chama. Lakini
Wema ndio kwanza mapenzi yake kwa chama yameimarika na sasa anaelekeza
nguvu zake kulikomboa jimbo la Singida mashariki kutoka CHADEMA na
kulirudisha CCM”, alisema Segamba.
No comments:
Post a Comment