SIKU Chache kupita baada ya Profesa Ibrahimu Lipumba kutangaza kujiuzulu nafasi ya uwenyekiti ndani ya Chama cha wananchi CUF, hatimaye Chama hicho kimeunda kamati ya mda itakayodumu kwa miezi sita ili kusimamia nafasi za uongozi .
Hatua
hiyo imetangazwa muda mfupi ulipita Jijini Dar es Salaam na Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara
baada ya kumalizika Kikao cha Dharula cha Baaraza la kuu la uongozi wa
chama hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa
Lipumba .
Seif
amesema katokana na Kanuni za CUF wamekubaliana kwa pamoja kuunda
kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi sita na baadae
kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya mwenyekiti.
Amesema
Kamati hiyo itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif
na mwenyekiti wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima na
Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na
kushirikiana na Vyama vyengine vinavyounda UKAWA ambapo anadai itakuwa
na jukumu lingine la kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.
No comments:
Post a Comment