Mkuu
wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Sisti Cariah (katikati) akiwaonyesha
waandishi wa habari utaratibu wa uhifadhi wa fomu za taarifa za wananchi
waliojiandisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, jana Alhamisi
(Agosti 27, 2015)Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Uchaguzi, Kailima Kombwey.
Afisa
TEHAMA katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adolf Kinyelo akitoa
ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mfumo uhifadhi wa taarifa za
wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura Alhamisi (Agosti 27,
2015) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC,
Kailima Kombwey.
Mkuu
wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dkt. Sisti Cariah akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari kuhusu uhakiki wa taarifa za wananchi katika daftari
la awali la wapiga kura Alhamisi (Agosti 27, 2015) Jijini Dar es
Salaam.
Watumishi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), David Charles (kushoto) na Ikabodi
Chimoto wakichapisha nakala za daftari la awali la uhakiki wa taarifa za
wananchi waliojiandisha katika la wapiga kura Alhamisi (Agosti 27,
2015) Jijini Dar es Salaam.
Mtumishi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Hassani Shamo akihakiki taarifa za
wananchi waliojiandisha katika la wapiga kura leo Alhamisi (Agosti 27,
2015) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Kombwey
akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP) Benedict
Wakulyamba daftari maalumu lenye taarifa za wanachi waliojiandisha zaidi
ya mara wakati wa zoezi la uandikishaji wa wananachi katika daftari la
kudumu la wapiga kura katika sehemu mbalimbali nchini Alhamisi (Agosti
27, 2015) Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), Kailima Kombwey
akiwaoyesha waandishi wa habari daftari maalum lenye taarifa za wanachi
waliojiandisha zaidi ya mara wakati wa zoezi la uandikishaji wa
wananachi katika daftari la kudumu la wapiga kura katika sehemu
mbalimbali nchini Alhamisi (Agosti 27, 2015) Jijini Dar es Salaam.
Na Anitha Jonas- MAELEZO.
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wananchi 52,078 waliojiandisha kwa
zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia
mashine za kieletroniki (BVR) wajisalimishe mara moja katika Ofisi za
Tume hiyo au kwa Wakurugenzi wa Halmashauri nchini kabla ya hatua kali
za kisheria kuchuliwa dhidi yao.
Aidha
NEC inatarajia kuyakabidhi majina ya watu wote waliowekewa pingamizi ya
uraia wakati wa zoezi la uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu
la wapiga kura kwa Idara ya Uhamiaji kwa ajili ya uthibitisho wa uraia
wao hapa nchini.
Akizungumza
na waandishi wa habari Alhamisi Agosti 27, 2015, Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Kailima Kombwey amesema Ofisi yake
imekabidhi orodha ya majina hayo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini
(IGP) Ernest Mangu kwa ajili ya kuwachulia hatua mbalimbali za kisheria
dhidi ya wananchi hao.
Kwa
upande Kamshina Msaidizi wa Jeshi la Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba
alisema Ofisi yake imeyapokea majina hayo na itaanza mara moja zoezi la
uchuguzi ikiwemo kuwahoji watuhumiwa hao ili kujua sababu ni ya kufanya
vitendo hivyo kinyume na sheria ya uchaguzi..
Akizungumzia
zoezi la uandikishaji wapiga kura katika mfumo wa BVR lililomalizika
hivi karibuni nchini, Kombwey alisema NEC imeandikisha zaidi ya wananchi
milioni 23.7 nchi nzima kwa kutumia mfumo wa BVR, ambapo taarifa zao
zimehifadhiwa katika sehemu tano ambazo ni BVR Mashine, kompyuta mpakato
(Laptop), Kadi ya kumbukumbu (VCD) na diski mweko (flash disk) pamoja
na kifaa maalum cha kuweka taarifa (Server).
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa uchaguzi alisema katika kila kitambulisho cha
mpigakura kilichotolewa na mfumo wa BVR kina taarifa mbalimbali ikiwemo
za NEC na sehemu aliyojiandikisha, tarehe aliyojiandikisha, na namba
BVR mashine iliyotumika kujiandikisha pamoja majina la mwandishaji
,hivyo kwa wale wanaosema kuna vitambulisho bandia vimekamatwa ni vyema
waviiwasilishe katika ofisi ya NEC kwa ajili kuvifanyia uchunguzi au
uhakiki.
Katika
hatua nyingine, Kombwey alitoa ufafanuzi juu ya suala la vyama vya
siasa kuzingatia ratiba zao za kampeni, pamoja na kuwepo na mgongano wa
taarifa kuhusu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kunyimwa
uwanja wa jangwani kwa ajili ya kufanyia uzinduzi wa kampeni zao Agosti
29, mwaka huu.
“Vyama
vyote vya siasa vilikuwa na uongozi wa NEC na kujadili juu ya ratiba
zao za kampeni na Chadema walisema uzinduzi wa kampeni zao ni tarehe
29/08/2015 katika jiji la Dar es Salaam lakini hawakuonyesha ni wapi
watafanya kampeni hizo ila kama wameambiwa uwanja wa jangwani
umeshachukuliwa basi watafute uwanja mwingine katika eneo lolote la
ndani ya jiji la Dar es salaam”, alisema Kombwey.
Naye
Mkurugenzi wa Tehama wa NEC Dkt. Sisti Kariah alisema Tanzania ni nchi
ya tatu katika Bara la Afrika kutumia mfumo wa BVR na mfumo huo ni mzuri
kwani una uwezo mkubwa ikiwemo uhifadhi wa taarifa zote
zilizoandikishwa katika mfumo huo.
No comments:
Post a Comment