Katibu wa TUICO Mkoa wa
Mbeya, Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na wajumbe wa Tuico siku ya
uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Otu jijini
Mbeya.(JAMIIMOJABLOG)
|
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa pamoja. |
CHAMA
cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na
Ushauri Mkoa wa Mbeya, kimefanikiwa kupata viongozi wapya watakao
kiongoza chama hicho katika kipindi cha miaka mitano 2015 hadi 2020.
Uchaguzi
umefanyika katika chuo cha wafanyakazi (OTU) jijini Mbeya na
kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Taasisi za serikali na binafsi
ambao wanawakilisha chama hicho cha (TUICO) mkoa wa Mbeya.
Akizungumzia
uchaguzi huo, Katibu wa TUICO Ndugu Merboth Kapinga, amesema uchaguzi
huo umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za chama hicho
ambacho zinaeleza kuwa kila baada ya miaka mitano ni lazima chama
kichague viongozi wapya.
Amesema,
wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo
vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana
na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote
mbili.
Amesema,
wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo
vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana
na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote
mbili.
Hata
hivyo amewataka viongozi hao kujenga uwezo wa kupambana na migogoro ya
kifedha kwani ndio changamoto kubwa inayowakabili wafanyakazi na
waajiri.
Aidha
amesisitiza kuwa , wafanyakzi ni lazima wawajibike kwanza halafu ndio
tudai haki nzetu kama vile nyongeza ya mshahara na motisha mbalimbali.
Viongozi
hao waliopatikana ni Mwenyekiti wa chama hicho, Willium Mhando pamojana
na wajumbe wa kamati tendaji, Boniface Mwanyamba kutoka kampuni ya
vinywaji baridi ya Pepsi , Joyce Mwakifuna kutoka kampuni ya Coca Cola
kwanza.
Wengine
ni Mwanaidi Thadei na Michael Msovakumwao wajumbe kitengo cha biashara,
sekta ya fedha, Winifrida Kinyakisu na Mohamed Tangulia.
No comments:
Post a Comment