Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Hiiti Sillo (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya TFDA
Dar es Salaam leo, wakati akitoa tahadhari ya uwepo katika soko wa
vipodozi vyenye viambato vilivyopigwa marufuku na Serikali. Kulia ni
Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu.
Mkurugenzi
wa Dawa na Bidhaa Nyongeza, Fimbo Mitangu (kushoto), akizungumza
katika mkutano huo huku akionesha moja ya kopo lenye kipodozi
vilivyopigwa marufuku. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uendelezaji Huduma wa
TFDA, Chrispin Severe
Mkurugenzi
wa Usalama wa chakula, Raymond Wigenge (kushoto) na Mkurugenzi wa
Huduma za Maabara wa TFDA, Charys Ugullam (kulia), wakiwa kwenye mkutano
huo na wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
1. MAMLAKA
ya Chakula na Dawa (TFDA) ni Wakala wa Serikali ulio chini ya Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii wenye jukumu la kudhibiti ubora, usalama na
ufanisi wa bidhaa aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
2. TFDA
inautaarifu umma kuwa kupitia mfumo wake wa ufuatiliaji ubora na
usalama wa bidhaa kwenye soko, imebaini uwepo wa vipodozi vyenye
viambato vilivyopigwa marufuku aina ya “steroids” zinazojulikana
kitaalam kama “clobetasol propionate”, “hydrocortisone” na “triamcinolone”.
3. Jumla ya Vipodozi aina tofauti 36 vya jamii ya krimu (creams) na
losheni (lotion) vimebainika kuwa na viambato hivyo vilivyopigwa
marufuku baada ya kufanya uchunguzi wa kina wa
matoleo 57 yaliyochukuliwa kwenye soko na viwanda vilivyotengeneza.
4. Vipodozi
hivyo vimetengenezwa na makampuni manne (4) yaliyoko hapa nchini na
kiwanda kimoja (1) kilichoko nje ya nchi kama ifuatavyo:-
Na.
|
Jina la kiwanda
|
Idadi ya vipodozi
|
Idadi ya matoleo
|
1.
|
Chemi & Cotex Industries Limited - Dar es Salaam
|
6
|
7
|
2.
|
Mamujee Products Limited - Tanga
|
11
|
20
|
3.
|
Tanga Pharmaceutical & Plastics Limited - Tanga
|
15
|
24
|
4.
|
Tridea Cosmetics Limited - Dar es Salaam
|
3
|
5
|
5.
|
Johnson & Johnson (Pvt) Ltd, Rattray Road, East London, South Africa
|
1
|
1
|
Jumla
|
36
|
57
|
5. Steroids aina ya “clobetasol propionate”, ‘hydrocortisone’’ na “triamcinolone” hutumika
kama dawa kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi yajulikanayo kitaalam
kama eczema, herpes labialis, psoriasis, contact dermatitis, alopecia
areata, vitiligo, lichen sclerosus, lichen planus na mycosis fungoides.
Steroids hizi hazitakiwi kutumika zaidi ya wiki mbili na lazima mgonjwa
apate ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi.
6. Baadhi
ya madhara yanayotokana na kutumia dawa hizi ni pamoja na muwasho na
kuvimba kwa ngozi (allergic contact dermatitis), ngozi kuwaka
moto (burning sensation), ngozi kukatikakatika (skin cracking), ngozi
kubabuka (fissuring) ngozi kukosa chembembe aina ya melanin inayoleta
kinga na hivyo kuifanya ngozi kuwa nyeupe isivyo kawaida
(hypopigmentation), madhara kwenye mifupa
(osteoporosis), kizunguzungu (dizziness), ngozi kukauka (skin
dryness), shinikizo la damu kwenye macho (glaucoma), vinyweleo vya
ngozi kupata athari (folliculitis), kuwashwa mara kwa mara (excessive
itching, pruritus, erythema and irritations), vidole kufa ganzi
(numbness of fingers), ngozi kusinyaa (skin atrophy) na ngozi
kubanduka (skin peeling/maceration). Madhara
mengine ni pamoja na ngozi kuwa nyekundu (skin redness), kusikia
kichefuchefu (nausea), kichwa kuuma (headache), kushindwa kupata
usingizi (insomnia), kutoka jasho jingi (sweating), kupata chunusi kubwa
kwenye ngozi (acne), kuchoka (fatigue), kuongezeka uzito (weight gain),
mapigo ya moyo kutoenda sawa (uneven heartbeats) na kuona maluweluwe
(blurred vision).
7. Kufuatia
hali iliyojitokeza na kwa kuzingatia madhara yanayoweza kusababishwa na
matumizi ya steroids kwa muda mrefu, TFDA imechukua hatua zifuatazo:
a. Kuzuia
kwa muda wa miezi sita (6) utengenezaji wa vipodozi aina ya krimu,
losheni na jeli kwenye viwanda vinne (4) vilivyohusika.
b. Kuwaelekeza
wenye viwanda vilivyohusika kuviondoa vipodozi vilivyokutwa
na steroids kwenye soko na kuviteketeza kwa gharama zao wenyewe.
c. Kufuta usajili wa vipodozi 31 vilivyokuwa vimesajiliwa.
d. Kuwaelekeza
Mameneja wa Ofisi za Kanda za TFDA kufanya ukaguzi katika maeneo yao
kwa kushirikiana na Ofisi za Halmashauri ili kuondoa katika soko
vipodozi vyote vilivyohusika.
8. Pamoja na hatua hizo, TFDA inatoa maelekezo yafuatayo:-
a. Wananchi
wote wasitumie vipodozi husika kwa kuwa vina madhara ya kiafya.
Wananchi wanaaswa kuangalia lebo za vipodozi walivyonavyo majumbani na
wakiona vina majina yaliyoainishwa waache kutumia vipodozi hivyo mara
moja.
b. Wasambazaji
na wauzaji wote kurudisha vipodozi vilivyohusika kwa watengenezaji au
kwa waliowauzia ili hatua za uteketezaji ziendelee.
9. TFDA
inaendelea kufuatilia vipodozi vingine vyote ili kujiridhisha na ubora
na usalama wake kwa watumiaji. Vile vile itaendelea na kazi yake
iliyopewa ya kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakikisha bidhaa
aina ya chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba zinazotengenezwa hapa
nchini au kuingizwa kutoka nje ya nchi ni bora, salama na zenye ufanisi
unaotakiwa.
10. TFDA
itawachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na
uvunjaji wa Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Sura 219 na
inawaomba wananchi wote kuendelea kutoa taarifa pale wanapobaini uwepo
wa bidhaa (chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba) duni au bandia kwenye
soko la Tanzania.
ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOBAINIKA KUWA NA VIAMBATO VILIVYO PIGWA MARUFUKU
Na.
|
Jina la kipodozi
|
Namba ya usajili
|
Toleo
|
Tarehe ya kuishamatumizi
|
Sehemusampuliilipochukuliwa
|
Aina ya kiambatokilichokutwa
|
Chemi&Cotex Industries Limited, Dar es Salaam
| ||||||
1.
|
Lovely Body Cream - Lemon
|
TAN15 CP 0095
|
12&16
|
Feb-18
|
Kwenye soko&Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
2.
|
Baby Soft Body Lotion
|
Haijasajiliwa
|
08
|
Dec-16
|
Kwenye soko
|
ClobetasolProprionate
|
3.
|
Siri Moisturizing Cream- Cocoa Butter
|
TAN13 CP 3118
|
26
|
Jan-18
|
Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
4.
|
Siri Moisturizing Cream- Lemon
|
TAN13 CP 3120
|
03
|
May- 18
|
Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
5.
|
Lovely Body Cream - Lemon
|
TAN15 CP 0094
|
16
|
Mar-18
|
Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
6.
|
Lovely Body Cream - Papaya
|
TAN15 CP0096
|
10
|
May-18
|
Kiwandani
|
Hydrocortisone
|
Mamujee Products Limited, Tanga
| ||||||
7.
|
Beauty Care Aloe Vera Beauty Cream
|
Haijasajiliwa
|
00283
|
Sep-15
|
Kwenye soko&Kiwandani
|
ClobetasolProprionate
|
8.
|
BOSS Hand & Body Lotion
|
TAN 15 CP 0300
|
10/0077258
|
No comments:
Post a Comment