KAMPUNI inayoandaa Tamasha la
kuombea amani kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka,
imetaja mikoa itakayoomba amani kuelekea uchaguzi Mkuu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema tamasha hilo kabla ya
kuelekea mikoani, litaanzia jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Taifa,
litakalofanyika Oktoba 4 jijini humo.
Msama alisema itikadi
za vyama vya siasa ni nyingi ni
lazima tuwe na umoja ili kuzungumzia suala hilo ambalo Mataifa mbalimbali
duniani hawana amani hasa katika vipindi vya uchaguzi.
Msama alisema tuweke tofauti
zetu pembeni na kumkimbilia Mungu atupitishe kwa amani katika kipindi cha
uchaguzi Mkuu.
Aidha Msama alisema kuelekea
uchaguzi Mkuu waimbaji, Boniface Mwaitege na Christopher Mwahangila
wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo huku Kamati ya maandalizi
ikiendelea na taratibu za kufanikisha tamasha hilo.
Kauli mbiu ya tamasha hilo ni
Tanzania ni ya kwetu, Tuilinde na kudumu amani ya nchi yetu ambayo
inachochea kufikisha ujumbe wa neno la Mungu.
Msaa aliitaja baadhi ya mikoa
itakayofikiwa na tamasha hilo ni pamoja na Morogoro, Iringa, Dodoma, Mbeya,
Shinyanga na Mwanza.
No comments:
Post a Comment