Sudan Kusini imetambuliwa rasmi na
kamati ya kimataifa ya Olimpiki na hivo kuruhusiwa kushiriki katika
Olimpiki mwakani huko Rio de Janeiro.
Sudan Kusini ilipata uhuru
miaka mine iliyopita, na hivo haikuwahi tarehe ya mwisho ya kuweza
kuingia katika Olimpiki ya London ya 2012.Mkimbiaji wa Sudan Kusini, Guor Marial, alishiriki chini ya bendera ya Olimpiki.
Wawakilishi wa Sudan Kusini walitokwa machozi nchi yao ilipokubaliwa kuwa mwanachama wa Olimpiki na kuwa mwanachama 206.
No comments:
Post a Comment