SIMBA YAFANYA KWELI TENA MBELE YA WAGANDA - LEKULE

Breaking

16 Aug 2015

SIMBA YAFANYA KWELI TENA MBELE YA WAGANDA

Kelvin Ndayisenga (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake goli la kwanza
Kelvin Ndayisenga (katikati) akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake goli la kwanza
Kiosi cha ‘Wekundu wa Msimbazi’ Simba kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 mbele ya timu ya URA FC ya Uganda kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jioni ya jana ikiwa ni mchezo wa kujipima nguvu na kujiandaa kwa ajili ya michuano ya ligi kuu Tanzania bara inayotaraji kuanza mapema mwezi ujao.
5
Simba ndio walikuwa wakwanza kupata goli kwenye mchezo huo dakika za mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji anaefanya majaribio kwenye timu hiyo Kelvin Ndayisenga aliyefunga goli la kwanza dakika ya nne ya mchezo.
Simba vs URA 5
Goli hilo halikudumu kwa muda mrefu kwani URA FC walisawazisha goli hilo dakika chache baadae mfungaji akiwa ni Kalanda Frank akitumia makosa ya mlinda mlango wa Simba Peter Manyika Jr aliyeukosa mpira wakati akitaka kuudaka na kutoa mwanya kwa Frank kuupachika mpira wavuni kuisawazishia timu yake.
Simba vs URA 4
Kipindi cha kwanza kilimalizika huku timu hizo zikiwa sare kwa kufungana goli 1-1 magoli ambayo yalifungwa kipindi cha kwanza.
IMG_7543
Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko kwa kuwatoa wachezaji wengi walionza kwenye mechi hiyo ambapo wengi wao walikuwa ni wale wasiopata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza huku wakiingia wale ambao mara nyingi wameonekana wakicheza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
3
Mabadiliko hayo yalirejesha uhai kwa Simba kutokana na mpira kubadilika kwa kiasi kikubwa ambapo Simba wakaanza kucheza pasi fupifupi kitu kilichoonekana kuwachanganya wachezaji wa URA.
Simba vs URA 9
Wakati mchezo ukielekea ukingoni, mlinzi wa kati wa Simba Juuko Murshid aliifungia timu yake goli la pili na la ushindi kwenye mchezo wa jana na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa Simba SC kushinda kwa goli 2-1 dhidi ya URA.
Juuko Murshid (kulia) akishangilia pamoja na Ibrahim Ajibu baada ya kuifungia timu yake goli la pili
Juuko Murshid (kulia) akishangilia pamoja na Ibrahim Ajibu baada ya kuifungia timu yake goli.

No comments: