NYOTA WA CAMEROON ASAINI MIAKA MITANO TOTTENHAM HOTSPUR - LEKULE

Breaking

16 Aug 2015

NYOTA WA CAMEROON ASAINI MIAKA MITANO TOTTENHAM HOTSPUR

Tottenham imetangaza kumsajili Mcameroon Clinton N'Jie kutoka Lyon kwa ada ya Pauni Milioni 10
KLABU ya Tottenham Hotspur ya Ligi Kuu ya England imethibitisha kumsajili mwanasoka wa kimataifa wa Cameroon, Clinton N'Jie kutoka klabu ya Lyon ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 10 ambayo italipwa baada ya kuruhusiwa kucheza.Mshambuliaji huyo chipukizi wa Simba Wasiofungika, atalipwa Pauni Milioni 1.5 baada ya kusaini Mkataba wa miaka mitano na klabu ya White Hart Lane.
Kocha wa Spurs, Mauricio Pochettino amelazimika kuongeza watu katika safu yake ya ushambuliaji ili kuiongezea makali kabla ya dirisha kufungwa Septemba 1, mwaka huu.
Na N'Jie anatarajiwa kuisaidia sana Spurs kutokana na umahiri wake katika safu ya ushambuliaji.
Kinda huyo aliyezaliwa Agosti 15, mwaka 1993 hadi sasa tayari ameichezea mechi 11 Cameroon na kuifungia mabao sita. Alijiunga na Lyon mwaka 2010, baada ya kusukiwa mipango na kaka wa beki wa zamani wa timu hiyo, Jean-Jacques Nono.

WASIFU WA CLINTON N'JIE
Kuzaliwa: Agosti 15, 1993
Ameicheza mechi 11 Cameroon na kuifungia mabao sita
Alijiunga na Lyon mwaka 2010 kwa msaada wa kaka wa beki wa zamani wa timu hiyo, Jean-Jacques Nono. Novemba 2012 aliichezea mechi ya kwanza Lyon akitokea benchi timu ikishinda 3-0 dhidi ya Reims, kabla ya msimu uliopita kung'ara katika Ligue 1, akifunga mabao nane katika mechi 33 za mashindano yote 15 tu akianza

No comments: