Sami Khedira nje miezi miwili - LEKULE

Breaking

4 Aug 2015

Sami Khedira nje miezi miwili

Kiungo wa klabu ya Juventus Sami Khedira atakua nje ya uwanja kwa miezi miwili.
Khedira aliyesajiliwa na vibibi vizee hivyo vya turin akitokea klabu ya Real Madrid alipata maumivu ya mfupa wa paja katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Marseille ya Ufaransa.
Huu ulikua ni mchezo wa kwanza kwa nyota huyu wa Ujerumani toka asajiliwe bure katika timu hiyo.
Hii ni mara ya pili kwa mchezo huyo kusumbuliwa na maumivu hayo ambapo mara ya kwanza ilikua ni katika mzunguko wa pili wa ligi ya Hispania la liga.Khedira aliisaidia timu ya taifa ya Ujerumani kufika fainali ya michuano ya dunia iliyofanyika nchini Brazil huku akikosa mchezo mmoja dhidi ya Argentina.


No comments: