Rais wa Gabon ametoa urithi wake kwa vijana wa Gabon
Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba ameahidi kutoa urithi wake wote kwa vijana nchini humo.
Ali
anasema kuwa mali yote aliyopokea kama urithi kutoka kwa babake mzazi
aliyekuwa rais wa Gabon kwa kipindi kirefu,Omar Bongo itakwenda kwa
vijana wa Gabon.
Shirika
la habari la AFP limesema kuwa rais Bongo ameahidi kuuza mijengo miwili
iliyoko Ufaransa aliyopewa na babake kwa thamani ya Franka moja kama
ishara ya kujitolea kuimarisha hali ya kiuchumi ya vijana wa taifa.
Jumba moja la kifahari lililoko katika mji mkuu wa taifa hilo litabadilishwa na kuwa chuo kikuu cha Umma.
Majumba mengine mawili yako mjini Paris Ufaransa.
Majumba mawili yako mjini Paris Ufaransa na lingine liko Gabon.
Kauli
hiyo ya rais Bongo inawadia wakati ambao majaji nchini Ufaransa wamekuwa
wakifuatilia na kuchunguza chanzo cha mamilioni ya fedha zilizotumika
kununua na kujenga majumba ya kifahari nchini humo.
Wapinzani
na wanaharakati wa kupambana na ufisadi wanasema kuwa huenda rais Ali
Bongo Ondimba ameona kibano kinachokuja akaamua kuirejeshea taifa mali
yake.
Shirika
la kupigana na ufisadi, Transparency International liliwasilisha kesi
mahakamani likitaka majaji hao waamuru kuwa mali ya umma ilitumika
kujistawisha wakati wa utawala wa babake marehemu rais Omar Bongo.
Babake marehemu rais Omar Bongo alitawala nchi hiyo kwa miaka 40.
No comments:
Post a Comment