Baadhi
ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa
watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok,
Jumatatu Agosti 17, 2015.
Na RFI
Idadi ya
watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Bangkok,
imeongezeka na kufikia 21, huku watu 125 wakiripotiwa kujeruhiwa. baadhi
ya raia kutoka China, Hong Kong, Malaysia na Singapore ni miongoni mwa
waliouawa.
Uraia wa
baadhi ya miili iliyopatikana, haujafahamika. Hata hivyo, polisi
imemtambua mtuhumiwa mmoja kupitia kamera za usalama ziliowekwa kwenye
eneo takatifu kwa watu kutoka jamii ya Hindu ambapo bomu lililipuka.
Wizara ya ulinzi ya Thailand inasema kuwa watu waliotega mabomu katika eneo takatifu jijini Bangkong waliwalenga watalii.
Wizara
hiyo imeongeza kuwa inawasaka waliotega mabomu hayo yaliyolipuka
Jumatatu jioni wiki hii na kusabisha vifo vya watu 21 na wengine 120
kujeruhiwa.
Eneo hilo
lililongwa limekuwa kivutio kikubwa cha watalii na raia wa nchi hiyo
ambao hufika katika eneo hilo linaloamiwa kuwa takatifu na dini la Hindu
kuomba bahati nzuri.
Hadi sasa haijafahamika ni akina nani waliotekeleza mashambulizi hayo na hakuna aliyejitokeza kudai kuhusika.
Waziri
Mkuu Prayuth Chan- ocha amesema kuwa serikali yake imeweka mikakati yake
kulipiza kisasi dhidi ya wale waliotekeleza mashambulizi hayo ambayo
pia anasema yalilenga kudhoofisha uchumi wa nchi hiyo.
Hii ndo ya mara kutokea kwa mashambulizi kama haya katika nchi hiyo inayoongozwa na wanajeshi.
No comments:
Post a Comment