Picha: Vigogo wa CCM Wajiunga Rasmi na CHADEMA Katika Ukumbi wa Mlimani City Mchana - LEKULE

Breaking

5 Aug 2015

Picha: Vigogo wa CCM Wajiunga Rasmi na CHADEMA Katika Ukumbi wa Mlimani City Mchana


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe(kushoto) akimkabidhi kadi ya chama hicho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida ambaye ni Mbunge wa zamani wa Iramba Mashariki Ndg.Mgana Msindai ambaye ametangaza kujiuzulu wadhifa wake, kujiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA. 
 
Msindai ni miongoni mwa wafuasi "watiifu" wa Mhe.Edward Lowassa. Inadaiwa wapo wenyeviti 15 wa CCM mikoa mbalimbali watajiunga na CHADEMA, baada ya Msindai kufungua njia.
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe(kushoto) akimkabidhi kadi ya chama hicho kwa Naibu Waziri wa Kazi Mh.Makongoro Mahanga.

Mbunge wa Arumeru Magharibi, Goodluck Olemedeye 

akikabidhiwa  kadi  ya chama cha Chadema na 

Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na 

maendeleo(CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe(kushoto) 


Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA), Mh.Freeman Mbowe(kulia) akimkabidhi kadi ya CHADEMA, Mh. Isaya Simon Bukakiye, (katibu wa Uchumi na Fedha Wilaya ya Kahama CCM)


No comments: