Baada
ya kusambaa sauti ya Nuh Mziwanda akimtongoza Wema Sepetu, muimbaji
huyo ameibuka na kukanusha kuwa sauti hiyo sio yake na kumtuhumu Wema
kuitengeneza sauti hiyo.
Akizungumza
na mtandao wa Bongo5 akiwa na mpenzi wake Shilole, Nuh amesema
kitendo kilichofanywa na Wema pamoja na timu yake sio cha kistaarabu.
“Mimi
nimetake easy, ni mambo ya dunia kwa sababu ni mambo ya dunia ambayo
yapo duniani. So wameamua tu kufanya vile sio suala ambalo lipo na sio
suala sahihi,” amesema Nuh.
“Ile
sio sauti yangu watu tu wameamua kufanya ili kunichafulia mimi labda na
mpenzi wangu. Kwa sababu ukisikiliza mwishoni kuna mtu amejitaja jina
lake. Ni kitu ambacho kimepelekwa studio wakaiweka sawa ili wapate kitu
kibaya kije kwangu na Shishi. Hiki kitu sikukitegemea kwa sababu watu
waliofanya kitu kama hicho ni watu ambao kwenye vitu vingi, kwenye mambo
ya kampeni yaani mimi sijategemea,” ameongeza.
“Mimi
hili suala nalichukulia kawaida na naona ni ushamba na upu*vu na hawana
akili hata kidogo. Kama ni kweli, angemfuata Shishi akamwambia kwamba
‘mpenzi wako kafanya kitu fulani fulani kwangu’ sio kutangaza.
"Na
kama kweli, kwanini asingesema wengine wanaomtongoza na akawaweka
mtandaoni? Ni Wema pamoja na watu wake wote ndio wamefanya hivi! Siku ya
kwanza Shishi alilipokea vibaya lakini baada ya kumuelewesha
kanielewa,” amesisitiza.
Kwa upande wa Shilole amekiri kulipokea jambo hilo kwa mshtuko lakini tayari ameshamsamehe Nuh na maisha yanaendelea.
“Mimi sina ugomvi na mtu katika maisha yangu,” amesema Shilole.
“Kama
wametengeneza ili wafanye hayo yote mimi sijali, watajua wenyewe, of
course limeathiri mapenzi yetu. Sasa hivi tupo fresh, kwasababu mwenyewe
ameshaniomba ‘mpenzi wangu samahani kwa kilichotokea lakini sio kweli.’
Nimeshamsamehe, mimi nimemuelewa alichosema Nuh basi.”
No comments:
Post a Comment