Mrema Ajitosa Tena Ubunge Vunjo - LEKULE

Breaking

15 Aug 2015

Mrema Ajitosa Tena Ubunge Vunjo


Mgombea ubunge jimbo la vunjo kupitia chama cha TLP Agustino Mrema akikabidhiwa fomu ya Ubunge.
Mgombea ubunge jimbo la vunjo kupitia chama cha TLP Agustino Mrema akikabidhiwa fomu ya Ubunge kutoka kwa Folgence Mponji.
Mwenyekiti wa chama cha TLP Agustino Lyatonga Mrema amechukua fomu ya kugombea ubunge katika jimbo la vunjo katika uchaguzi mkuu utaofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu  Mrema amesema kwamba jimbo la Vunjo ni mali yake na hayuko tayari kuona likichukuliwa na   wanasiasa wa umoja wa katiba ya Wananchi (Ukawa).
Alisema amelazimika kuchukua fomu ya kugombea jimbo hilo kutokana na maombi ya wananchi wa jimbo la vunjo wengi wao wakiwa wanawake ambao muda mwingi walikuwa wakimfuata nyumbani kwake wakimtaka agombee kutokana na rekodi nzuri  ya kulitumikia jimbo hilo.
Amedai kuwa propaganda zinazo enezwa na wapinzani wake wakidai kuwa yeye amezeeka na ni mgonjwa, nizakupuuzwa kwani kwa sasa yeye ana afya njema na anataka aitwe ‘bebi’. kama ambavyo vijana wa mjini wanavyosema “uzee mwisho Chalinze mjini  kila mtu baby”.
Aidha Mrema amesema  tayari amenunua gari la kusafirisha abiria  (coster) linalotumika katika jimbo hilo kusafirisha wakina mama wajawazito, shughuli za misiba pamoja na kubeba wananchi katika maeneo yao bila kuwatoza malipo.

No comments: