MO anogesha tamasha la Simba Day - LEKULE

Breaking

9 Aug 2015

MO anogesha tamasha la Simba Day

IMG_1602
Mgeni rasmi katika Tamasha la Simba Day, Mohammed Dewji akichukua taswira mbalimbali kwenye majukwaa yaliyofurika mashabiki na wanachama wa Simba katika tamasha hilo lililofanyika kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
IMG_1615
Mgeni rasmi katika Tamasha la Simba Day, Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa wadau kwenye jukwaa kuu wakati wa tamasha la Simba Day. Kulia mwenye pama ni Makamu wa Rais wa klabu ya Simba SC, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
IMG_1648
Rais wa klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva (kushoto) na Mgeni rasmi Tamasha la Simba Day, Mohammed Dewji wakisubiri kuingia uwanjani kwa ajili ya zoezi la kukagua vikosi vya Simba SC pamoja Sports Club Villa ya Uganda vilivyomenyana jana katika tamasha hilo.
IMG_1666
Mgeni rasmi wa tamasha la Simba Day, Mohammed Dewji “MO” akikagua na kusalimiana na kikosi cha wachezaji wa timu ya Sports Club Villa ya Uganda.
b17
Mgeni rasmi, wa Simba Day, Mohammed Dewji “MO”, akisalimiana na mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi.
IMG_1673
MO akiendelea na zoezi hilo kwa kikosi cha timu ya Simba SC.
IMG_1677
Mgeni rasmi Simba Day, Mohammed Dewji akielekea kwenye benchi la ufundi la timu ya Simba SC.
IMG_1679
MO akisalimia na Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic pembeni yake ni Rais wa klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva.
IMG_1680
Mgeni rasmi tamasha la Simba Day, Mohammed Dewji “MO” akisalimiana benchi la ufundi la Simba SC mara baada ya kukagua vikosi.
IMG_1681
MO akiwasalimia wanachama wa Simba na mashabiki waliofurika katika uwanja wa Taifa jana jijini Dar es Salaam.
IMG_1682
Mgeni rasmi tamasha la Simba Day, Mohammed Dewji “MO” akiwa amefuatana na Rais wa klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva kuelekea jukwaa kuu mara baada ya kukagua vikosi.
IMG_1686
Meza kuu ikiangali mtanange uwanjani.
RAIS wa klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva, (pichani juu), jana alikuwa kama kocha wa Chelsea, Josse Morinho, kutokana na jinsi alivyokuwa akiwaelekeza wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba dhidi ya timu ya soma ya wasanii wa Bongo Movie na Bongo Flava kwenye maadhimisho ya siku ya Simba almaarufu kama Simba Day.
Aveva ambaye alikuwa “kaulamba” yaani kapiga suti yake nyeusi, alikuwa ndio “kocha wa timu hiyo ya viongozi wa Simba.
Akiwa amevalia suti nyeusi, hakuweza kutulia kwenye kiti, kila wakati alisimama na kuwaelekeza wachezaji wake kwa kunyoosha mikono na kufoka.
Timu ya soka ya viongozi wa Simba iliibuka mshindi wa bao 1-0.
Baada ya pambano hilo, lilifuatia tendo la kuwatambulisha wachezaji wapya wa Simba na benchi la ufundi kabla ya kuanza kwa pambano maalum la kirafiki baina ya timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na wageni wao Sports Club Villa ya Uganda, katika pambano hilo la kirafikli, Simba iliibanjua Sports Club Villa “Jogoo” bao 1-0. Bao lililofungwa na Awadh Juma, kwenye dakika ya 45 ya kipindi cha lala salama.
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia)
timu ya Bongo Movie na Bongo Flava zikichuana.

Kikosi cha timu ya wasanii
Kikosi cha timu ya viongozi wa Simba na wachezaji.
Aveva katika “ubora” wake.
Bongo Flava na Bongo Movie wakitoana jasho uwanjani kabla ya mechi rasmi ya Simba SC na Sports Club Villa ya Uganda.
Ben Kinyaiya, (kulia) wa timu ya wasanii, akiumiliki mpira mbele ya Imani Kajula
JB akiwatoka wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba.
JB akifuatilia jinsi wenzake wanavyopelekwa puta na timu ya viongozi wa Simba.
Kocha mkuu wa Simba, katika “ubora” wake
Kocha Mkuu wa Simba, akizungumza jambo na mchezaji wake, Hamisi Kiiza Diego.
Michezo mbalimbali ikiendelea kusherehesha Simba Day.
Kikosi cha timu ya Sports Club Villa, kilichomenyana na Simba na kuangukia “pua” kwa kunyukwa bao 1-0
Kikosi kipya cha Simba, kilichoinyuka Sports Club Villa.
Mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao.
Aveva katika “ubora” wake.
Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, ni mmoja wa watu “waliovunjwa mbavu” na Aveva
Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, (kushoto), akionyesha “kumbe wamo”
Imani Kajula, (kulia), wa timu ya viongozi wa Simba, akijaribu kuutuliza mpira.
Mchezaji wa kiungo wa timu ya Wasanii JB, akiusaka mpira katikati ya uwanja.
Ibrahim Masoud, “Maestro” akipiga hesabu wakati wa pambano kati ya timu ya soka ya viongozi wa Simba na ile ya wasanii.
Mshambuliaji wa Simba, Khamisi Kiiza “Diego”, (kulia), akijaribu kuupiga mpira huku akichungwa na msitu wa walinzi wa SSC Villa kutoka Uganda.

No comments: