MGOMBEA urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, anatarajiwa kujulikana leo baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kupendekeza jina la mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Jana Kamati Kuu ya chama hicho ilikutana jijini Dar es Salaam, kujadili majina ya wagombea wa nafasi ya urais na ubunge.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba alisema kamati hiyo imekutana kwa ajili ya kujadili ajenda tatu ikiwemo ya kujadili majina ya wagombea.
Alisema kujadiliwa kwa majina hayo ni baada ya kumalizika kwa kura za maoni zilizofanyika katika mikoa mbalimbali nchini.
No comments:
Post a Comment