...Akikata utepe kama ishara ya uzinduzi huo.
...Akiwa tayari amepanda gari la mwendo wa haraka baada ya uzinduzi.
Mgeni rasmi, Hawa Ghasia, akizungumza jambo.
Mstahiki Meya wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Didas Massaburi (kushoto), akisalimiana na Sadick Mecky Said kabla ya uzinduzi.
Gari la mwendo wa haraka likiwa limepaki sehemu ya uzinduzi huo.
Moja ya magari ya mwendo wa haraka ambalo ni fupi.
Baadhi ya wananchi wakitamani kuyaona magari hayo.
Baadhi ya wafanyakzi wa DART na wananchi wakisikiliza taaarifa iliyokuwa ikisomwa kwa mgeni rasmi kabla ya uzinduzi.
Madereva wa Kichina waliokuja kwa ajili ya kutoa mafunzo ya udereva wa magari hayo ya mwendo wa haraka.
Kamanda
wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Dar es Salaam, Suleiman Kova
(kushoto) akiwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed
Mpinga.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo kwenye uzinduzi huo.
Mwonekano wa ndani moja ya magari hayo.
Baadhi ya wakazi wa eneo la Kimara wakiyashudia magari hayo yalipotua kituoni hapo.
Hawa Ghasia akishuka kwenye moja ya magari hayo mara baada ya kumaliza safari ya kutokea Ubungo-Kimara.
Baadhi ya wananchi waliopata fursa ya kuyapanda magari hayo kutokea Kimara wakiteremka kituo cha Ubungo.
Viongozi walioshiriki uzinduzi huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kushuka katika moja ya magari hayo.
MABASI ya mwendo wa haraka jijini Dar es
Salaam yamezinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, akiambatana na viongozi
mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said.
Uzinduzi huo wa huduma ya mpito (interim
service) umefanyika leo katika kituo cha DART kilichopo nje ya kituo
kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.
Akizungumza na wananchi na wanahabari waliohudhuria hafla hiyo, Hawa
Ghasia alisema kuwa jiji la Dar es Salaam ni la pili katika kutekeleza
mradi huo baada ya Afrika ya Kusini.
Alisema kuwa wananchi wapokee huduma hiyo mpya ya usafiri kutokana
hali halisi ya kwenda na wakati tofauti na kuendelea kutumia huduma
ambazo haziko kiteknolojia zaidi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said, akizungumza
katika hafla hiyo amesema huduma hiyo itawawezesha wananchi kupunguza
idadi ya magari yanayopita barabarani kwa wingi kwa kupanda gari moja tu
la DART ambalo litakuwa ni kubwa lenye kutoa usafiri wa haraka.
Aidha amewataka wananchi kuwa makini wakati wanapokuwa barabarani
hasa zile ambazo zitakazokuwa zikitumika kwa magari hayo ya mwendo wa
haraka, akisema wananchi yeyote atakayepita katikati ya barabara hizo na
kusababisha ajari atachukuliwa hatua kali hata kama gari la mwendo wa
haraka litamgonga, kwani yeye ndiye atakayeonekana mwenye makosa kama
ambavyo treni linapogonga mtu au gari.
“Mwananchi yeyote atakayepita katikati ya barabara hizi na
kusababisha ajali atachukuliwa hatua kali mara moja na hata kama gari la
mwendo wa haraka litamgonga, yeye ndiye atakayeonekana mwenye makosa
huku akifananisha na barabara ya treni.”
No comments:
Post a Comment