Jaji Mstaafu, Damian Lubuva.
Kwanza nimshukuru Mungu kwa kuweza kutupa uhai leo na kujiona tuko katika nchi yetu iliyojaa amani.
Naamini
kwamba katika maeneo yote ya nchi, wazalendo wa nchi hii walijitokeza
bila kulazimishwa kwenda kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura (BVR)kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu unaotarajiwa
kufanyika Oktoba 25.
Mkoa wa
mwisho kuhitimisha rasmi kazi hiyo iliyoanza kwa kusuasua mwanzoni mwa
mwaka huu ni Jiji la Dar es Salaam.Kabla ya uandikishaji, tayari Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (Nec) ilikuwa imekadiria kwamba mwaka huu kutakuwa na
watu milioni 24 wenye sifa za kujiandikisha na hatimaye kushiriki
katika uchaguzi huo wa kuwachagua madiwani, wabunge na rais.
Kwa
dalili zinavyojionesha, idadi hiyo ya watu milioni 24 inaweza isifikiwe
kwa sababu ya matatizo yaliyojitokeza wakati wa uandikishaji ambayo
yaliwakatisha tamaa baadhi ya watu kutokana na usumbufu uliokuwepo.
Hata
hivyo, kama idadi hiyo itakaribiwa, itakuwa si haba na jambo muhimu
baada ya hapo ni waliojiandikisha kuhakikisha kila mmoja anapiga kura.
Unapopiga kura ndipo unapoonesha uzalendo wako, kwani unasababisha
kupatikana kwa kiongozi bora, usipopiga kura elewa kwamba unachangia kwa
kiwango cha juu kusimika viongozi wasiofaa katika nchi hii yenye
changamoto nyingi za maendeleo.
Nimesema
hivyo kwa sababu kumeanza kutokea tatizo la watu kutotaka kupiga kura na
badala yake kutumia zoezi la uandikishaji kupata vitambulisho tu, yaani
ile kadi ya mpiga kura kugeuzwa kitambulisho.
Nilisikitika sana kuona katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, zaidi ya nusu ya waliojiandikisha kupiga kura hawakupiga kura, hii ilinisikitisha sana na kwa kweli yule ambaye hakupiga kura ajiambie katika nafsi yake kwamba hakuitendea haki nchi yetu.

Hili ni
tatizo kwa sababu kila aliyejiandikisha anatakiwa kupiga kura. Kutopiga
kura maana yake ni kuacha masuala muhimu ya nchi yaamuliwe na wachache
badala ya walio wengi na ambao hawakupiga kura wakati walikuwa
wamejiandikisha mwaka 2010 wajue kwamba walichangia kupata viongozi
wabovu katika nchi hii.
Najua
kwamba zoezi la uandikishaji wapiga kura ulikuwa na kasoro nyingi na za
kukera kwa wananchi waliojitokeza. Baadhi ya matatizo hayo yalikuwa ya
kujirudia kiasi kwamba wengine walianza kuhoji kama wahusika wanajifunza
kutokana na mwenendo wa mchakato mzima wa uandikishaji.
Naamini
kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Mstaafu, Damian Lubuva na
serikali kwa ujumla itakuwa imejifunza kutokana na mchakato huu na taifa
litajiepusha na mkanganyiko kama huu kwenye chaguzi zijazo.
Binafsi nitafurahi kuona idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura wanafanya hivyo. Tunajua kuwa katika chaguzi nyingi duniani, si rahisi kwa watu wote waliojiandikisha kupiga kura wapate fursa ya kupiga kwa sababu tofauti.
Lakini, kama tunavyoona kwa jirani zetu wa Kenya, tunaweza walau kupata wapiga kura waliofika asilimia 75 ya waliojiandikisha.

Katika
baadhi ya nchi za wenzetu, wako wananchi ambao husafiri kutoka Ulaya na
Marekani kwa lengo la kuwahi kupiga kura nchini mwao, huo ni uzalendo
ambao nasi tunatakiwa kuujenga.Watanzania hawawezi kuacha kupiga kura
kwa sababu yoyote ile. Kama unataka kiongozi unayemtaka ashinde katika
uchaguzi, unatakiwa kupiga kura.
Watu
wengi wakipiga kura, hata uongozi unaoingia madarakani unakuwa na amani
kwa vile unafahamu umeingia kwa mamlaka ya walio wengi. Ndani ya moyo
wako weka dhamira kwamba ‘uchaguzi mkuu wa mwaka huu ni lazima nipige
kura’, vinginevyo wote watakaoacha kupiga kura wataonekana ni wasaliti
wa nchi yao wasio wazalendo.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.
No comments:
Post a Comment