Vitanda
mbali mbali vya Hospitali vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation
ya nchini Canada, ikishirikiana na Jumuiya ya TAQWA Tanzania, kwa ajili
ya Hospitali Kisiwani Pemba kabla ya kukabidhiwa kwa uongozi wa Wizara
ya Afya Pemba.(Picha zote na Hanifa Salum, PEMBA.)
Maboksi
mbali mbali yenye madawa kwa ajili ya Hospitali pamoja na mikoba ya
Watoto mayatima, vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation ya nchini
Canada, ikishirikiana na Jumuiya ya TAQWA Tanzania, mikoba kwa aajili ya
wanafunzi wa skuli.
WANANCHI
mbali mbali wakiangalia Vitanda, Boksi za madawa, baskeli za
walemavu,Magongo ya watu wenye ulemavu, pamoja na Standi za kutundukia
dripu, Vilivyotolewa na Jumuiya ya Qamer Foundation ya Nchini Canada,
ikishirikiana na Jumuya ya TAQWA Tanzania.
WANANCHI
mbali mbali wa jimbo la Ole na shehia jirani, wakiwasikiliza kwa makini
viongozi mbali mbali wa Serikali na Jumuiya ya TAQWA Tanzania pamoja na
Qamer Foundation ya Nchini Canada, kabla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo
kwa wananchi hao.
WAZIRI
wa Katiba na Sheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwakilishi
wa Jimbo la Mgogoni Pemba, Aboubakar Khamis Bakar wa pili kushoto akiwa
na mwakilishi wa jimbo la Ole Hamad Massoud Hamad, pamoja na viongozi wa
Jumuiya ya TAQWA Tanzania na Jumuiya ya Qamer Foundation ya Nchini
Canada.
MWAKILISHI
wa Jimbo la Ole kisiwani Pemba Hamad Masoud Hamad, akizungumza katika
hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda vya Hospitali,
vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole kisiwani Pemba.
MKURUGENZI
mtendaji wa Jumuiya ya TAQWA Tanzania Dk.Salha Mohamed Kassim,
akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo Vitanda
vya Hospitali, vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole kisiwani
Pemba.
Mkurugenzi
Mkuu mtendaji wa Jumuiya ya Qamer Foundation kutoka Canada Balkis
Alhadad, akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbali mbali ikiwemo
Vitanda vya Hospitali, vigari vya walemavu, mikoba ya skuli huko Ole
kisiwani Pemba.
BAADHI
ya wanachama wa Jumuiya ya Qamer Foundation kutoka Canada, wakimvisha
mkoba wa skuli mtoto yatima, ambae ni mwanachama wa jumuiya y tahafidh
Quran na Maendeleo ya Kiislamu ya Jimbo la Ole.
No comments:
Post a Comment