Jeshi la Nigeria linasema kuwa
limewaokoa zaidi ya watu 180, wengi wao wanawake na watoto, kutoka kwa
kundi hatari la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram, katika jimbo la
Borno.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, msemaji moja wa
jeshi amesema kuwa kambi kadhaa za waasi hao zilizoko karibu na mji wa
Maiduguri zimeharibiwa na kamanda mmoja wa Boko Haram kukamatwa, lakini
duru hizo hazijasema ni lini tukio hilo lilifanyika.Wakati hio huo, Rais wa Niger, Mahmadou Issoufou, amesema kuwa jeshi jipya linalojumuisha wanajeshi kutoka mataifa kadhaa huko Afrika magharibi, lina uwezo mkubwa wa kukabiliana na Boko Haram.
No comments:
Post a Comment