Maafisa wa polisi nchini Uhispania
wamemkamata raia mmoja wa Morroco baada ya nduguye ambaye alikuwa
anasafrishwa hadi nchini Uhispania ndani ya sanduku kukosa hewa na nusra
afariki.
Watu hao walikuwa wakiabiri feri kutoka eneo la
Uhispania la Melilla kaskazini mwa Afrika hadi katika mji wa Bandari wa
Almeria kusini mwa Uhispania wakati mzee huyo alipogundua kwamba nduguye
hapumui na kuwashauri wafanyikazi wa feri hiyo.Licha ya kujaribu kumfufua mtu huyo alifariki.
Maafisa wa polisi wamemshtaki nduguye ambaye alikuwa akisafiri kwa kutumia pasipopti ya Ufaransa kwa mauaji ya kutokusudia.
No comments:
Post a Comment