Jana ikiwa ndio ni siku ya Mwisho kuchukua na Kurejesha Fomu za Urais,Ubunge na Udiwani Katika Majimbo Yote ya Uchaguzi Nchini,Chama Cha Mapinduzi Kimeanza Vema Harakati Hizo baada ya Aliekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Abdallah Dadi Chikota (pichani) kupita bila kupingwa kuwa Mbunge wa Jimbo jipya la Nanyamba,Mkoani Mtwara
Hatua
hiyo Imetokea baada ya wagombea wawili wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo(CHADEMA) Na aliekuwa Mgombea wa Chama cha Wananchi CUF
Kutojitokeza Kurudisha Fomu zao hadi Muda Uliopangwa na Tume ya Uchaguzi
Kumalizika. Wagombea hao ambao walichukua Fomu na Kutorejesha ni
Severin Simon Magwaya (CHADEMA) na Twahil Saidi Namwaga wa CUF.
Jimbo
la Nanyamba katika Halmashauri ya Wilaya Ya Mtwara ni Jimbo Jipya Baada
ya Kugawanywa Jimbo la Mtwara Vijijini Abdallah Dadi Chikota Ambae Hivi
karibuni Aliagana na Wasaidizi wake wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Licha kuanza Harakati zake Za Kisiasa Aliwaomba Kutekeleza Vema
Utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa Mkoa wa Lindi.
Chikota
akibainisha Baadhi ya Miradi Hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Wodi ya Kisasa
pamoja Nyumba ya Ghorofa itakayokaliwa na Familia 10 za Waganga katika
Hospital Ya Sokoine Lindi,Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Kilwa
na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa
Kufuatia
Kutotokea kwa Wagombea hao jana Sasa Inasubiriwa Taratibu za Tume ya
Uchaguzi Kumtangaza Rasmi kuwa Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Mkoani Mtwara
No comments:
Post a Comment