Carolina Chilele ashinda milioni 20 za "Mama Shujaa wa Chakula" - LEKULE

Breaking

23 Aug 2015

Carolina Chilele ashinda milioni 20 za "Mama Shujaa wa Chakula"



Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula shindano linaloendeshwa na shirika la Oxfam kupitia programu yake ya Grow ambapo kauli mbiu ni Wekeza kwa wakulima wanawake wadogo wadogo inalipa lafika tamati ambapo kulikuwa na mchuano mkali kati ya washiriki 15 ambao walikuwa katika Kijiji cha Kisanga, Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani wakiwa na shughuli mbalimbali za Kilimo ambazo zililenga hasa katika kuwakomboa wakulima wadogo wadogo wanawake wadogo wadogo. Washiriki hao walikaa kijijini kwa muda wa siku 21 hatimaye kufikia kumpata mshiriki mmoja ambaye amejishindia kiasi cha shilingi 20,000,000/= fedha ambazo zitanunua pembejeo za Kilimo. Fainali hizo zilifanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam

Afisa Kilimo Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dkt. Kissa Kajigili , akiwapongeza Oxfam kwa kuandaa shindano la Mama Shujaa wa Chakula na washiriki wote kwa ujumla walioshiriki katika Shindano hilo, Pia alimpongeza Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2015 Carolina Chilele na kumtaka awe mfano bora pia akawe chachu ya kuinua kilimo na kuwasaidia wenye uhitaji yaani wakulima wanawake wadogo wadogo, Mwisho aliwaomba Oxfam waendelee na shindano hili muhimu.

Jackson Yusuph Mzumba Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kibweni akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Serikali ya Kijiji cha Kisanga.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Kisarawe Bw. Ellioth Phillemon Mwasambwite akiwashukuru Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 , na kuwaaaga rasmi, pia kumpongeza Mshindi wa Shindano hilo msimu wa Nne Bi. Carolina Chilele , Mwisho aliwapongeza Oxfam kwa kuanzisha shindano endelevu kwa Maendeleo ya wakulima hasa wanawake.

Mmoja wa akina mama ambao walikuwa wanakaa na Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula katika Kijiji cha Kisanga Bi. Sophia Shomvi akitoa neno la Shukurani kwa washiriki hao kwa jinsi walivyo kaa vizuri pamoja na pia kuwaachia elimu kubwa wanakijiji hao. Mwisho alitoa neno la Kuwaaga Rasmi.

Kiongozi wa Timu ya Urasimishaji ardhi vijijini kutoka Wizara ya Ardhi nyuma na Maendeleo ya Makazi Bw. Swagile Msananga akiwapongeza washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, pia kwa mshindi wa Shindano hilo kwa msimu wa Nne 2015 Bi. Carolina Chilele kwa ushindi wake na kumtaka kuwa mfano Bora kwa jamii kwa ujumla, Pia alisisitiza watu sio kuwa tu na ardhi lakini pia kupata umiliki wa ardhi walizonazo.


Baadhi ya Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 wakipewa tuzo za ushiriki wao na Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster 

Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2015 msimu wa Nne Carolina Chilele akipongezwa na washiriki mwenzake 

Picha ya pamoja 




Baadhi ya wageni waalikwa, wafanyakazi wa Oxfam, ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika sherehe za fainali za shindano la Mama Shujaa wa Chakula.

Bi. Hawa Mkata aliyekuwa mshiriki kutoka Mtwara akitoa neno la shukurani kwa wanakijiji wote ambao waliishi nao kijijini kwa Muda wa Siku zote 21, na zaidi zile familia ambazo wao wamekuwa nao kwa kipindi chote cha Shindano hilo. Mwisho aliwaomba washiriki wenzake kujua kuwa wote ni washindi lakini mmoja ndio kawawakilisha kwa kuchukua zawadi ile ya milioni Ishirini.

Eva Mgeni, Mshiriki kutoka Bagamoyo Kutoka Mkoa wa Pwani, Akitoa shukurani zake kwanza kwa Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow ambayo kauli mbiu yake ni kuwekeza kwa wakulima wadogo wadogo wanawake inalipa kwa kuendesha shindano hili na kuwa kupitia washiriki wa shindano hilo wamejifunza mambo mengi na ya kimaendeleo, Mwisho aliwashukuru wanakijiji wote kwa ushirikiano wao na moyo wa ukarimu katika kipindi chote wakiwakKijijini.

Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa salam zake za Shukurani kwa wote waliofanikisha shindano la Mama Shujaa wa Chakula kwenda vizuri tangu mwanzo mpaka mwisho, aliwashukuru wanakijiji cha Kisanga kwa kukubali kwao shindano lifanyike katika kijiji hicho pia aliwapongeza washiriki wote wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula na kuwasihi kuwa wote walikuwa ni washindi, Mwisho alichukua nafasi hiyo kumpongeza mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 na kumsihi aende kuwa mfano wa kuigwa kwa wakulima wenzake pia akawe balozi mzuri na kuiwakilisha vema Oxfam

Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2015 msimu wa nne akitoa neno la Shukurani kwa ushindi alioupata. Ameshukuru shirika la Oxfam kwa kuendesha shindano hilo na kuahidi kuwa atakwenda kuwa Balozi mzuri na kusema kuwa washiriki wote ni washindi na yeye amepata zawadi hiyo kuwawakilisha wote.

Burudani ikiendelea 

No comments: