Dar es Salaam.
Chama cha ACT – Wazalendo kitazindua kampeni zake za uchaguzi kwa kuwatambulisha wagombea wote wa ubunge waliosimamishwa kwenye majimbo ya Tanzania –Bara na Zanzibar. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 30 katika Uwanja vya Zakhem Mbagala, wilayani Temeke kuanzia saa nne asubuhi.
Chama cha ACT – Wazalendo kitazindua kampeni zake za uchaguzi kwa kuwatambulisha wagombea wote wa ubunge waliosimamishwa kwenye majimbo ya Tanzania –Bara na Zanzibar. Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika Agosti 30 katika Uwanja vya Zakhem Mbagala, wilayani Temeke kuanzia saa nne asubuhi.
Katibu
wa Mipango na Mikakati wa ACT – Wazalendo, Habibu Mchange aliwaambia
waandishi wa habari jana kwamba maandalizi ya uzinduzi huo yanaendelea
vyema na kwamba hafla hiyo itahudhuriwa na viongozi wote wa kitaifa wa
chama hicho wakiwamo Kiongozi wa Chama, Zitto Kabwe na Mwenyekiti wake,
Anna Mghwira ambaye pia ni mgombea urais.
“Baada
ya mwenyekiti wetu, Mama Mghwira kuchukua fomu ya kugombea urais,
Watanzania wamekuwa na shauku ya kutaka kujua mustakabali wetu kuelekea
Uchaguzi Mkuu,” alisema na kuongeza: “Hivyo basi tunawakaribisha
wananchi wote siku hiyo waje kushuhudia kampeni za kisayansi. Ndiyo
maana tumeamua kuwaita wagombea ubunge wote kuhudhuria na kuwatambulisha
rasmi kwa Watanzania.”
Alisema ACT – Wazalendo
imejipanga kuchukua dola na kuleta siasa safi, tofauti na vyama vingine
akisisitiza kuwa kina nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo ya Watanzania.
Hivyo kuwataka wananchi kuhudhuria.
Alisema katika
siku ya uzinduzi, kwa mara ya kwanza wabunge waliohama kutoka vyama vya
CCM, CUF na Chadema watazungumza, pia wataendelea kuinadi ilani ya
uchaguzi wa chama hicho. Alisisitiza kuinadi kaulimbiu ya chama hicho ya
utu, uadilifu na uzalendo.
Katibu wa Fedha na
Rasilimali ya chama hicho, Peter Mwambuja alisema pia kimejipanga
kufanya siasa za malengo na masuala kwa maendeleo ya Watanzania siyo
kupiga propaganda.


No comments:
Post a Comment