NEC yaongeza siku za kujiandikisha Dar - LEKULE

Breaking

31 Jul 2015

NEC yaongeza siku za kujiandikisha Dar


Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeongeza siku nne zaidi za kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Mkoa Dar es Salaam.
Uamuzi huo umechukuliwa ili kukidhi mahitaji ya kuandikisha watu wote wenye sifa.
Awali, uandikishaji ulitarajia kumalizika leo, lakini kutokana na nyongeza ya siku hizo, sasa kazi hiyo itafikia tamati Agosti 4.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema Tume imefikia uamuzi huo baada ya kuona watu wengi wakiendelea kujitokeza kujiandikisha, huku pia muda uliopangwa ukikaribia kumalizika.
“Watu wengi wamejitokeza na kwa jinsi hali ilivyo, tumeona ni vizuri tukaongeza muda hadi Agosti nne,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema NEC imezingatia hali halisi ilivyo kutokana na mlundikano wa mambo kama utoaji wa fomu za urais, uteuzi, wingi wa watu jijini na kuona ni vyema kuongeza muda wa uandikishaji.


No comments: