Mdosi mmoja ambaye ni
bosi wa kampuni moja ya kusafirisha mafuta jijini Dar aliyefahamika kwa
jina la Jetti anasakwa na polisi kwa RB; CHA/RB/5871/2015 SHAMBULIO LA
MWILI akidaiwa kumfanyia kitu mbaya deveva wake aitwaye Deogratius.
Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa
kutokea Julai 18, mwaka huu maeneo ya Mbagala Mission jijini Dar ambapo
dereva huyo alipigwa, akajeruhiwa ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno
kabla kukoswakoswa risasi.
Chanzo ni nini?
Akisimulia mkasa huyo, Deogratius
alidai: “Siku ya tukio nilikuwa natokea Kongo nikiwa nimeongozana na
gari nyingine ya kampuni. Kwa kuwa nilikuwa na usingizi, nilipofika
Iringa nilipumzika lakini mwenzangu akaendelea na safari. Asubuhi
nikaondoka.
“Nilipofika Mikumi (Morogoro) nililiona
lile gari la mwenzangu limeanguka, nikasimama na kwenda kuangalia lakini
sikuona mtu, nikapiga simu ofisini kuwajulisha lakini bosi mmoja
akaniambia wanazo taarifa, mimi nirudi tu ofisini.
“Nilipofika ofisini usiku saa moja
nikashangaa bosi wangu mmoja anakuja na kunishika kwa staili ya
‘Tanganyika jeki’ huku yule bosi wangu Mhindi akinipiga ngumi, mateke na
kitako cha bastola.
“Damu zilinitoka sana, nilipouliza kwa
nini napigwa wakadai kuwa eti mimi nimemtorosha dereva mwenzangu yule
aliyepata ajali Mikumi, jambo ambalo niliwakatalia.
“Bosi akachomoa bastola na kufyatua
risasi hewani, nilipoona vile nikaanza kukimbia ndipo aliponifyatulia
mbili lakini zilinikosa, moja ikapiga kwenye kioo cha ofisi yake.
“Walinikimbiza na kunikamata kisha
wakaendelea kunipiga hadi usiku walipokuja wafanyakazi wengine na
virungu, kwa kipigo kile nilipoteza fahamu.
“Niliposhituka nikajikuta kwenye gari
lenye vioo ‘tinted’, niligundua tupo mitaa ya Upanga. Nikapata akili ya
kuchukua simu yangu na kuwasiliana na ndugu zangu ambapo wakati
nikifanya hivyo, wale watu waligeuza gari na kunirudisha Kituo cha
Polisi Chang’ombe.
“Kufika pale wakatoa maelezo yao na kwa
kuwa ndugu zangu walishafika pale, wakanisaidia kupata fomu ya matibabu
kutoka polisi ‘PF3’, nikaenda kutibiwa.
“Julai 19 ndipo wakaja viongozi wa Chama
cha Madereva wa Malori Tanzania (CHAMAMATA) na kunichukua tena mpaka
Kituo cha Polisi cha Chang’ombe ambapo niliandikisha maelezo na kupewa
RB; CHA/RB/5871/2015 SHAMBULIO LA MWILI,” alieleza Deogratius kwa
masikitiko.
Akaelezwa kuwa upelelezi kuhusiana na
tukio hilo unaendelea na tayari watuhumiwa wawili wamekamatwa ila bosi
aliyekuwa kimbelembele (Mdosi) na wengine hawajakamatwa.
Waandishi wetu walifanya jitihada za
kumpata bosi huyo Mdosi ambapo alipopigiwa simu alizuga kisha akatoa
namba ya simu ya mtu mwingine na kutaka apigiwe huyo kwani ndiye mwenye
ufafanuzi. Naye alipopigiwa hakutoa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment