Mapenzi Yamtokea PUANI Davina - LEKULE

Breaking

24 Jul 2015

Mapenzi Yamtokea PUANI Davina


Staa wa Filamu za Kibongo, Halima Yahaya amedaiwa kutoswa na mwanaume aliyemuachanisha na mumewe ambaye alikuwa bosi wake kwenye kampuni moja iliyopo Kinondoni jijini Dar.

Chanzo cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kimedai kuwa, baada ya Davina kuzinguana na mumewe kisa kikiwa ni bosi huyo (Jina tunalihifadhi kwa sasa) alifunguliwa ofisi maeneo ya Kinondoni jijini Dar kisha maisha yakaendelea.

“Si unakumbuka kuna yule mwanaume ambaye ndiye alimzuzua Davina hadi akaachana na mumewe? Basi baada ya pale Davina alifungiliwa ofisi yeye na Mike (Sangu) iliyokuwa inajihusisha na mambo ya TV ya mtandaoni, mambo yakawa bambam, akasahau hata machungu ya ndoa yake kuvunjika.

“Lakini sasa hivi mambo yameharibika, yule kibosile katibuana na Davina, kaamua kuchukua kila kitu katika ofisi ile na kuiacha tupu.

Mike ambaye ndiye aliyemshawishi Davina waanzishe hiyo ofisi sasa hivi yuko zake mkoani anampigia debe mgombea wake,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:

“Sasa hivi Davina anahaha, anajuta kuachana na mumewe.”

Davina alipovutiwa waya na kuulizwa juu ya madai ya kutoswa na mwanaume aliyevunja ndoa yake alisema amechoshwa na maneno ya watu kwani hajawahi kuwa na uhusiano na bosi wake huyo.

“Mh! Watu wananitungia habari jamani mimi sipendi kwa sababu hawajui tu wanavyoniharibia, sijawahi kuwa na uhusiano na bosi wangu, kuhusu kazi mbona bado naendelea na hivi ninavyokwambia naelekea hapo kazini,” alisema Davina.


Akizungumzia ishu hiyo, Mike Sangu aliyekuwa akifanya kazi ofisi moja na Davina alisema: “Hayo mambo ya Davina kuwa na uhusiano na mkurugenzi wetu siyajui, ninachojua kwa sasa tumesimama kidogo kwa sababu tunafanya usaili wa watu ili tufungue televisheni kwa ujumla kwani mwanzo ilikuwa TV Online na hata huyo Davina tumemuambia alete CV,” alisema Mike.

No comments: