MADEREVA
nchini wametishia kufanya mgomo kwa mara nyingine kuanzia wiki ijayo na
kwa muda usiojulikana iwapo serikali kupitia kamati iliyoundwa
kushughulikia matatizo yao haitawaita na kuongea nao kuhusu posho zao za
ndani na safari za nje.
Kauli
hiyo imetolewa jijini dar es Salaam jana na Katibu mkuu wa Chama cha
Madereva, Rashid Salehe ambapo alisema madereva hao wamemtuma na kuitaka
serikali isimuulize kiongozi yeyote wa madereva kipindi watakapoamua
kugoma mpaka madai hayo yatekelezwe.
Alisema
kuwa pamoja na kupata mikataba mipya katika kikao cha mwisho
kilichofanyika mwezi uliopita hata hivyo bado madereva wanaendelea
kupewa mikataba mingine tofauti na ile waliokubaliana katika kikao hicho
cha mwisho.
“Madereva
bado wanaendelea kupata shida na kusota bila kujua hatima ya posho zao
za safari za ndani na nje hivyo tunaitaka Wizara ya mambo ya Ndani na
Wizara ya Kazi isije kutuita viongozi na kutuuliza juu ya hili kwa kuwa
madereva hao wamechoka hivyo wamenituma baada ya kufanya ziara za mikoa
kadhaa na kuniagiza niseme kuwa wataacha kuendesha magari kama serikali
haitawaita kujua hatima ya suala hilo” alisema Salehe.
Aliongeza
migogoro kati ya madereva na matajiri wa magari hayo ni kutokana na
mfumo wa viongozi wa serikali kuhusika kuwafanya biashara hiyo huku
wakiwa wanawakandamiza waliochini.
“Kuna
kampuni ya magari fulani sitayataja jina tajiri wake analugha za matusi
na tumeshamrekodi wakati akitoa matusi hayo na tunafikiria kumpeleka
huyu bwana mahakamani” alisema Salehe.
Alisema
kuwa pia kuna gari la kigogo mmoja ambalo lilibeba sumu za mgodini
limekwama porini muda mrefu na tajiri wa basi hilo amewatelekeza
madereva hao bila kujali afya zao zinaendelea kuharibika kwa kukaa na
sumu hiyo.
Salehe
alisisitiza kama mfumo uliopo wa vigogo wa sarikali kuwa ndio wamiliki
wa mabasi hayo basi kila watakalo kuwa wanafanya litaonekana la kitoto
na migogoro haitaisha na ukizingatia wanalindwa na sheria ya mwaka 1955
ambayo wanaitumia mpaka leo.



No comments:
Post a Comment