
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka mwanasiasa mkongwe, Kingunge-Ngombale Mwiru kufanya anachotaka kufanya.
Juzi
Kingunge alijitokeza hadharani na kuzungumzia na waandishi wa habari
huku akiwaambia kwamba kilichofanywa na CCM katika kumpata mgombea wa
urais, Dk. John Magufuli ni haramu.
Dalili
ya CCM kupasuka vipande zimeanza kuonekana dhahiri, baada ya Kingunge
kujitokeza hadharani kupingana na maamuzi yote yaliyofanywa hususani
kukata jina la Edward Lowassa katika hatua za mwanzo za kuteua mgombea
urais.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (pichani), akizungumza na
mtandao huu jana kuhusu tuhuma zilitolewa na Kingunge ambaye kadi yake
ya uanachama ni namba nane, alijibu kwa kifupi kwamba afanye anachotaka
kufanya na kwamba hana maoni zaidi.
“Sina
Comment (maoni) wewe unataka niseme nini? kaandike hivyo nilivyosema
kwa sababu na mimi ni mwandishi na nilishawahi kuwa mhariri kwa hiyo
najua,” alisema na kukata simu.
Chama
hicho tawala kilimteua Dk. John Magufuli na Samia Suluhu Hassan kuwa
mgombea wake mwenza kupeperusha bendera yake katika uchaguzi mkuu wa
Oktoba mwakani.
Jumla
ya watia nia 38 majina yao yaliingia katika vikao vya awali, lakini
waliovuta kuingia tano bora ni Magufuli, Dk. Asha-Rose Migiro, Balozi
Amina Salum Ali, Januari Makamba na Bernard Membe.
Hata
hivyo, Halmashauri Kuu (NEC) iliwachuja Makamba na Membe na kuwabakiza
Magufuli, Amina na Migiro kisha Magufuli kuibuka mshindi


No comments:
Post a Comment