
Staa
wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel ambaye jina lake la Kiislam baada ya
kubadili dini ni Rahma, hivi karibuni alifanya maulidi ya kumtoa mwanaye
Cookie lakini katika hali ya kushangaza alifanya mambo ambayo
yaliwatibua Waislam.
Aunt alifanya tukio hilo hivi karibuni
nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar kisha kuwaalika ndugu, jamaa na
marafiki ambapo mbali na kuombewa dua na maustadhi, pia aliwafuturisha
Waislam waliokuwa kwenye mfungo.
Licha ya kitendo hicho kilichodaiwa
kuteketeza milioni kadhaa za fedha kupongezwa na wengi, katika hali ya
kushangaza kuna mambo ambayo ilibainika yalikwenda kinyume na taratibu
za dini ya Kiislam.
Kwanza
Aunt baada ya kutokea kwenye hadhara
akiwa na mwanaye, alikuwa kavalia shela lilioacha wazi sehemu ya juu ya
kifua na kimtandio ambacho baadaye kiliondoka na kumuacha kichwa wazi,
kitu ambacho ni kinyume na Uislam.
Pili
Katika tukio hilo kulikuwa na ratiba ya
kukata keki ambapo ulipofika muda wa yeye kumlisha mwanaume aliyezaa
naye (Moze Iyobo), alimpa kwa staili ya ‘njiwa’, jambo ambalo
halikutarajiwa kufanyika katika mazingira yale.
Tatu
Mjadala mwingine ulihusu Aunt kugandana na Moze Iyobo kama mume na mke wakati mtoto huyo wamempata nje ya ndoa.
Baada ya kuona na kusikia malalamiko ya
baadhi ya wageni waalikwa kuhusu sherehe hiyo, mwandishi alimtafuta
Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar, Alhad Mussa Salum ambaye alionesha
kushangazwa na jambo hilo na kusema ni makosa na kufanya hivyo ni
kuchezea dini ya Mwenyezi Mungu.
“Mtu anayefanya mambo hayo ni kwamba
huko ni kuchezea dini ya Mwenyezi Mungu, watu wanatakiwa kuelewa kwamba
utukufu wa Mwezi wa Ramadhani ni usiku na mchana. Kama kuna staa kafanya
hivyo, amemkosea sana Mungu,” alisema shehe mkuu.


No comments:
Post a Comment