IYOBO NA AUNTI MAHABA NIUE ZENJI....! - LEKULE

Breaking

31 Jul 2015

IYOBO NA AUNTI MAHABA NIUE ZENJI....!


Aunt Ezekiel Grayson Gwantwa na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Mo’ wakijiachia.

MAHABA nifilisi. Aunt Ezekiel Grayson Gwantwa na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Mo’ wameonesha wazi kinachoitwa mapenzi ni kikohozi baada ya kujiachia kimahaba hadharani wakiwa sanjari na ‘mtoto wao’, Cookie jambo lililozua miguno mingi ya chinichini.

Moses Iyobo ‘Mo’ akimbeba mtoto wao Cookie

Wawili hao walinaswa hivi karibuni visiwani Zanzibar, ambako kulikuwa na tamasha maalum la filamu (ZIFF), ambapo Aunt alikuwa miongoni mwa waalikwa huku Iyobo ‘akivamia shamba la bibi’ kwa kile alichodai ni kumpa kampani mwandani wake.

“Unajua hii ndiyo safari yangu ya kwanza tangu nijifungue, kwa hiyo ni muda muafaka, ngoja tufurahie maisha kidogo jamani,” alisema Aunt.


No comments: