Batuli laivu na mwanaume! - LEKULE

Breaking

31 Jul 2015

Batuli laivu na mwanaume!


Muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ katika mahaba mazito na mchekeshaji Stan Bakora.


DAH! Wakati mashabiki wake wakiamini si mtu wa ‘kurukaruka’ kivile, muigizaji mwenye mvuto wa aina yake Bongo Movies, Yobnesh Yussuph ‘Batuli’ amekwaa aibu baada ya picha zake zikimuonesha akiwa kimahaba chumbani na mchekeshaji Stan Bakora kuvuja, mtandao huu unakupa mchapo kamili.

TUJIUNGE NA CHANZO

Chanzo kilichovujisha ubuyu huo kilieleza kuwa, kina picha zinazomuonesha Batuli akiwa kimahaba na Stan bila kujua walizipiga kwa ajili gani.

“Nina picha za Batuli akiwa na kanga moja, anaonekana yuko na Stan Bakora ‘on bed’, sijajua wamezipiga za nini ila ukiziona nadhani unaweza kuzifanyia kazi,” kilidai chanzo hicho.

Alipotafutwa Stan Bakora kuhusiana na picha hizo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Batuli, alisema:

“Ni muvi kaka, katika hali ya kuuvaa uhalisia ndiyo tulipiga kimahaba zaidi lakini sina uhusiano wowote na Batuli.




No comments: