Staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’.
Lagos, NigeriaSTAA wa muziki kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’amefungukia ujio wake mpya kupitia mitandao ya kijamii kuwa yupo mbioni kufanya kolabo na Rihanna.
Rihanna.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Davido aliulizwa na mashabiki baada
ya kufanya kolabo la kimataifa na rapa kutoka Marekani, Meek Mill
kupitia Ngoma ya Fans Mi, mashabiki watarajie nini ndipo alisema yupo
mbioni kutoa ngoma na Rihanna lakini hakuweka wazi mipango kamili
inayoendelea.Davido kwa sasa ni mmoja wa wasanii kutoka Afrika, anayewakilisha Nigeria kwenye Tuzo za MTV Africa (MAMA) akiwania vipengele vitatu sambamba na staa kutoka Tanzania, Diamond Platnumz.




No comments:
Post a Comment