Meneja huduma za jamii wa Airtel Bi. Hawa Bayumi akiongea na wwndishi wa habari (hawapo pichani).
Kampuni ya simu za mkononi
ya Airtel kupitia mpango maalumu wa Airtel Fursa, imeandaa warsha
maalumu ya mafunzo ya ujasiriamali na namna ya kuendesha biashara zao
kwa faida itakayofanyika mwanzoni mwa wiki ijayo.
Warsha hii itakayowajumuisha
vijana kati ya miaka 18 - 24 wenye nia ya kujifunza na kujikwamua
kiuchumi, inategemea kufanyika Jumatano ya tarehe 22/7/205, katika
ukumbi wa Golden Rose hotel ulioko Arusha mjini kuanzia saa 2 asubuhi.
Akiongea na waandishi wa
habari Meneja huduma za jamii wa Airtel Bi. Hawa Bayumi alisema, "Airtel
Fursa imeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia na kuwawezesha vijana wengi
nchini kupata elimu na pia kuwapatia misaada itakayowawezesha kuendesha
biashara zao kwa ufanisi"
Mpaka sasa tumeshafanya
semina kama hizi katika mikoa ya Dar es Saalam na Mwanza na kuwawezesha
vijana zaidi ya 500 kupata mafunzo hayo muhimu ikiwemo usimamizi wa
mtaji, mbinu za masoko, kuzitambia fursa na ujuzi wa kibiashara, namna
ya kuendesha biashara na kuweka mahesabu, jinsi ya kufungua akaunti
benki na nyingine nyingi"
Aliongeza kwa kusema "Kwa
wakazi na vijana wa Arusha hii ni zamu yao sasa, tunatoa wito,
wajitokeze kwa wengi kua mafunzo haya bure bila gharama yoyote kupitia
wataalamu wetu mahiri wenye ujuzi katika maswala ya biashara n
ujasiriamali"
Tunaamini vijana wengi
watatoka katika mafunzo haya wakiwa wamewezeshwa kuwa na mtazamo chanya
lakini zaidi wakiwa na mbinu za kuendesha biashara zao kwa mafanikio
zaidi.
Airtel kupitia Airtel Fursa
itatoa warsha kama hizi maeneo mbalimbali ya nchi ambapo baada ya warsha
hii kufanyika Arusha, wakazi na vijana wa mkoa wa Mbeya nao watafikia
na kupata mafunzo katika wiki 2 zijazo.


No comments:
Post a Comment