Dar es Salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa kampuni ya habari ya Nation Media Group (NMG), Joe Muganda ameahidi kusimamia kikamilifu weledi na uhuru wa vyombo vya habari vya kampuni hiyo, ambavyo ni pamoja na magazeti ya The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti yanayozalishwa na Mwananchi Communication Limited.
Ofisa Mtendaji Mkuu mpya wa kampuni ya habari ya Nation Media Group (NMG), Joe Muganda ameahidi kusimamia kikamilifu weledi na uhuru wa vyombo vya habari vya kampuni hiyo, ambavyo ni pamoja na magazeti ya The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti yanayozalishwa na Mwananchi Communication Limited.
Muganda alisema hayo
wakati akitambulishwa kwa wafanyakazi wa Mwananchi Communications
Limited na wadau wa habari. Mwananchi Communication Limited ya Tanzania
na The Monitor ya Uganda ni kampuni tanzu za NMG.
Muganda,
aliyeanza kazi na NMG takriban mwezi mmoja uliopita akichukua nafasi ya
Linus Gitahi, alisema kwa kipindi chote cha mkataba wake anapenda
kuongoza kampuni ambayo habari zake zinaaminika na kila mtu na kufanya
kazi kwa uhuru wa hali ya juu.
Muganda aliwaeleza wadau
waliohudhuria hafla ya utambulisho huo jijini hapa juzi kuwa wakati huu
wa uchaguzi, MCL haitafungamana na upande wowote na itaendelea kutoa
habari kwa uwajibikaji mkubwa.
“Uwajibikaji ni jambo la
msingi sana unapoongoza chombo cha habari kwa sababu iwapo ukikosea
kidogo unaweza kulipeleka taifa katika uelekeo mbaya,” alisema Muganda.
“Lazima
tuhakikishe habari ni ya kweli, inatenda haki kwa wote na kubwa zaidi
ni kuwa huru… hiyo misingi ndiyo nitakayoisimamia kikamilifu,” alisema
Muganda.
Ahadi hiyo aliirudia tena jana asubuhi wakati
akitambulishwa kwa wa wafanyakazi wa MCL kuwa wakati huu wa uchaguzi,
kampuni haitaegemea upande wowote hivyo uwajibikaji huo na weledi
utasaidia vyombo vyote vya kampuni hiyo kuaminika kwa wadau wake.
“Hatutakiwi
tuwe na tofauti na mamlaka. Tunachotaka ni kuwa huru kwa kila kitu
tunachokifanya na siyo kuambiwa nini tufanye… tutakuwa wazi, watenda
haki kwa kila mtu,” alisema Muganda huku akiwasihi wafanyakazi hao
kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya kampuni.
Katika
hafla ya juzi iliyohudhuriwa na wanahisa, wasomaji, watangazaji,
wafanyakazi wa MCL na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Muganda alisema
atajikita katika kuhakikisha anafanikisha matarajio ya wanahisa wa
kampuni hiyo.
Alisema ataweka mkazo katika kukuza vipaji vya vijana
watakaosaidia kusukuma gurudumu la maendeleo ya nchi na bara la Afrika
kwa ujumla. “Mara nyingi sana tumekuwa hatutilii maanani uendelezaji wa
mtaji wa nguvu kazi imara na yenye uweledi wa kutosha. Katika uongozi
wangu nitafanya kila niwezalo kuendeleza vipaji na nguvu kazi kwa
kuwashirikisha Watanzania kikamilifu,” alisema Muganda.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCL, Leonard
Mususa aliipongeza kampuni hiyo kwa kazi kubwa inayoifanya katika
kuandika habari za Uchaguzi Mkuu kwa kina na haraka hasa wakati wa
mchakato wa kumpata mgombea wa urais CCM.
Alisema
wakati wa kutafuta tano bora hadi anavyolala hakuwa amepata habari
yoyote ya matokeo, lakini alivyoamka asubuhi alikuta magazeti ya MCL
yameandika kiundani habari hiyo.
Mususa hakusita
kuendeleza na kilio cha kuiomba Serikali iliruhusu gazeti la The East
African lianze tena kusambazwa nchini baada ya Serikali kulifungia
Januari mwaka huu.
Mususa alisema soko la habari lina
changomoto lukuki ambazo zinafahamika bayana na wadau wake. “Hadi sasa
tunavyozungumza gazeti lililokuwa linapendwa nchini la The East African
bado limefungiwa. Tunaamini kuwa Serikali italifungulia ili lianze
kusambazwa tena nchini,” alisema.
“Nimeongea na wadau
mbalimbali juu ya hilo na hata viongozi waliopo serikalini wanalipenda
The East African…kwa chochote kilichotokea kisiwe tena sababu bali
tunatakiwa kuyamaliza na kuwarudishia wasomaji gazeti walipendalo.”
Alisema
kuna dalili za wazi kuwa hakuna kuaminiana kati ya vyombo habari na
Serikali hivyo tasnia ya habari inatakiwa kujenga uaminifu na uhusiano
mzuri na mamlaka kwa kuandika habari za kweli, haki na zisizoegemea
upande wowote.
Mususa alisema MCL inataka kuongeza
kiwango cha tabia ya kujisomea kwa kuwaomba wadau kutoa maoni juu ya
masuala wanayopenda kuyasoma ili yaweze kuandikwa kwa ubora na uweledi
wa hali ya juu.
Mkurugenzi Mtendaji wa MCL, Francis
Nanai alimuelezea Muganda kuwa ni “kiongozi mzuri ambaye tutanya naye
kazi vizuri kama yule aliyetoka (Gitahi)”.
No comments:
Post a Comment