WATU ZAIDI YA 800 WAPOTEZA MAISHA KWA JOTO KALI PAKISTAN - LEKULE

Breaking

25 Jun 2015

WATU ZAIDI YA 800 WAPOTEZA MAISHA KWA JOTO KALI PAKISTAN

Mmoja wa majeruhi wa joto nchini Pakistan akipatiwa huduma ya kwanza.


WATU zaidi ya 800 wamefariki dunia mpaka sasa kutokana na hali ya joto kali kwenye Mkoa wa Sindh uliopo kusini mwa nchi ya Pakistan.
Zaidi ya watu 780 wamefariki huko Karachi huku 30 wakiripotiwa kufariki kutoka sehemu nyingine mkoani humo.
Taarifa kutoka katika hospitali kadhaa mkoani humo zimeripoti kuelemewa baada ya mochwari zake kujaa miili hivyo kushindwa kuhifadhi miili mingine.
Mamlaka husika zimelaumiwa kwa kushindwa kukabiliana na janga hilo lililoanza Jumamosi iliyopita.
Leo, Jumatano imetangazwa kuwa siku ya mapumziko ili kutoa fursa kwa wananchi kubaki katika makazi yao ili kujikinga na joto hilo.

Jana, Jumanne joto lilipanda na kufikia nyuzi joto 45 (113F) ambapo Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Nawaz Sharif alizitaka mamlaka kuchukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo huku majeshi yakitawanywa kwa ajili ya kuweka vituo vya kupunguza joto kwenye maeneo mbalimbali.

No comments: