WALIMU
katika shule ya msingi Nambaza Kata ya Nansimo wilayani Bunda,
wamesema watahama shule hiyo endapo serikali ya wilaya hiyo haitachukua
hatua madhubuti kukomesha ushirikina shuleni hapo.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Sospiter Mafuru, alisema walimu wake wanafanyiwa
vitendo vya ushirikina ikiwa ni pamoja na kusumbuliwa usiku na
kunyolewa nywele sehemu za siri.
Alitaja
vitendo vingine kuwa ni kuvuruga vyombo vya ndani wakati wa usiku,
kumwaga michuzi na damu kwenye mashuka na nguo za walimu hao.
“
Vitendo hivi vimetishia usalama wa walimu hadi sasa walimu watatu wa
kike wamehama shule hii kwa hiyo tunaomba jamii ya Nambaza wachukue
hatua,”alisema.
Alisema
awali ushirikiana huo ulianza kwa wanafunzi kuugua na kuanguka ovyo
na baadaye kwa walimu na aliomba Serikali kuchukua hatua na kukaa na
wananchi wao.
Mafuru alisema hadi sasa ana walimu tisa,wa kike watano na wa kiume wanne.
Mkuu
wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, alisema tayari ameviagiza vyombo
vya dola kwenda kijijini hapo kufanya utafiti kuwabaini watuhumiwa hao.
No comments:
Post a Comment