SERGIO RAMOS ANAITAMANI MANCHESTER UNITED - LEKULE

Breaking

22 Jun 2015

SERGIO RAMOS ANAITAMANI MANCHESTER UNITED

Beki hodari wa klabu Real Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Sergio Ramos ameonyesha nia ya kutaka kuondoka ndani ya klabu yake na kuelekea Manchester United.
Inasemekana tangu atimuliwe kocha Anchelot, beki Ramos hana furaha ndani ya klabu hiyo huku akizidi kuwashtumu viongozi wa klabu hiyo kutokumjali pamoja na mchango wake mkubwa ndani ya Real Madrid.
Ramos mwenye umri wa miaka 29, amesema yupo tayari kwenda Manchester united muda wowote ikitokea hivyo. Pia Ramos amewalaumu viongozi wa klabu kwanza hawajataka kumuongezea mkataba ambao unaisha ndani ya misimu miwili ijayo.
Tarifa zinadi kueleza kwamba Ramos amekasirishwa kwa wachezaji wenzake kama Gareth Bale kuongezewa kiasi cha mshahara huku yeye akitupiliwa mbali na kuongeza kuwa klabu za nje zikionyesha nia ya kumtaka mmoja kati ya wachezaji wakubwa wa Madrid, basi Real Madrid imekuwa ikitoa neno kwamba haiuzi mchezaji lakini klabu ya Barcelona imeshatamka hadharani kwamba inamtaka beki huyo na viongozi wa Madrid wamenyamaza hivyo ni wazi hata klabu imemchoka.
Sergio Ramos licha ya mahasimu wake Barcelona kumuhitaji lakini yeye anataka kwenda kucheza ligi ya uingereza na anaitaka Manchester United.

No comments: