P DIDY ATUPWA JELA KWA MASAA KADHAA - LEKULE

Breaking

23 Jun 2015

P DIDY ATUPWA JELA KWA MASAA KADHAA

Jumatatu ya jana Mwanamuziki na mjasiria mali Sean John Combs a/k/a P Diddy alikiona cha moto baada ya kutupwa jela ya Chuo Kikuu cha California kwa muda kabla hajaachiliwa kwa dhamana.

Mapema siku ya jana Mwanamuziki huyo alifika maeneo ya chuo hicho na kwenda kumuangalia mtoto wake Justin Combs wakati afanya mazoezi ya mpira.

Wakati Mtoto Justin akiendelea na mazoezi pamoja na wenzake ghafla walirumbana na kocha wa timu yao, Sal Alosi, kitendo ambacho kilimfanya Mwanamuziki huyo kuingilia kati na kusababisha zogo kwenye eneo hilo.

Baada ya zogo hilo Kocha Mkuu wa timu ya Chuo hicho ndugu Jim Mora aliita polisi ambao walimtia nguvuni P Diddy na kwenda kumtupa rumande na baada ya mazungumzo kwa muda, Diddy aliachiliwa kwa dhamana ya dola elfu 50,000 huku kesi ikipangwa kusikilizwa tena July 13 mwaka huu.

No comments: