Toka tuzo za BET Awards 2015 zifanyike juzi jumapili ya tarehe 28 baadhi ya wasanii wakubwa kutoka Africa wamekuwa
wakijitokeza kueleza sababu za kwanini hawakutokea kwenye tuzo hizo
mwaka huu wakidai hawafurahishwi na kitendo cha kituo kikubwa cha
burudani Marekani BET kuwatenga wasanii wa Kiafrika na wasanii wengine wakubwa kwenye tuzo hizo, wakilalamika hawapendezwi na BET
kuwapa wasanii wa Kiafrika tuzo hizo backstage masaa machahce kabla ya
tuzo hizo kuruka Live nchini humo. Kitendo hiki kimeonekana kama dharau
kwa wasanii wa Kiafrica wanaojitahidi kwa uwezo na juhudi kuwakilisha muziki wao wa Kiafrika kwenye ramani ya soko la kimataifa.
Msanii kutoka Nigeria, Wizkid ameamua kuliongelea suala la yeye kuto kuwepo kwenye Tuzo hizo, akidai hatokaa aende kwenye Tuzo hizo kama BET wataendelea kuwapa wasanii wa Kiafrica
tuzo zao nyuma ya pazia na sio mbele ya watu wote duniani, yupo radhii
awe anafanya shows tu kwa ajili ya mashabiki wake lakini sio kwenda
kwenye tuzo za BET, huku akisisitiza kuwa anawapenda sana BET
na anatambua mchango wao wa kuwainua wasanii wa kiafrika ila kwa style
hii yupo radhii aende tu kama mtu mwengine wa kawaida kushududia tuzo
hizo.
BET hawajapendezwa na kitendo hiki, yakamfikia Wizkid alieamua kuelezea sababu za yeye kuto kuwepo siku ya jumapili.
No comments:
Post a Comment