Hai. Siku moja baada ya kuhukumiwa kulipa faini Sh1 milioni au
kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la shambulio la kawaida dhidi ya
aliyekuwa mwangalizi wa ndani wa uchaguzi mkuu uliopita, Mbunge wa Hai
na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza kuwania tena ubunge
katika jimbo hilo.
Mbowe aliyeepuka kwenda jela kwa
kulipa faini hiyo juzi, alitangaza uamuzi huo jana alipokuwa akihutubia
mkutano wa hadhara katika eneo la stendi ya zamani mji mdogo wa
Bomang’ombe, Kilimanjaro.
Mwenyekiti huyo alifikia
hatua hiyo baada ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo
kumshinikiza agombee ubunge na kumchangia Sh800,000 za kuchukua fomu
ambayo ndani ya Chadema hugharimu Sh250,000.
“Nashukuru
kwa walioanzisha wazo hili lakini zaidi ninawashukuru waliojitolea
kunichangia fedha. Nimekubali nitagombea ubunge katika uchaguzi ujao,”
alitangaza Mbowe na kufanya uwanja kulipuka kwa shangwe.
Mbowe
aliyeambata na wabunge kadhaa akiwamo Philemon Ndesamburo wa Moshi
Mjini, alijinasibu kuibuka na ushindi wa kishindo yeye na chama chake
katika uchaguzi ujao kuanzia jimbo la Hai na katika majimbo yote ya Mkoa
wa Kilimanjaro.
“Kama sheria ingekuwa inaruhusu
ningefurahi iwapo CCM ingesimamisha wagombea zaidi ya 10 katika Jimbo la
Hai ili wapambane na mimi kwa sababu mgombea mmoja pekee siyo saizi
yangu,” alijinasibu Mbowe.
Hukumu dhidi yake
Akizungumzia
hukumu iliyomtia hatiani na kuhukumiwa faini au kifungo, Mbowe ambaye
pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema alikusudia kwenda jela
kuwakilisha mamilioni ya Watanzania wanaosota huko “kwa kesi na hukumu
za kipuuzi”.
“Kama kesi ya mtu mwenye dhamana ya
uwakilishi wa wananchi kwa nafasi ya ubunge inaweza kuendeshwa kwa zaidi
ya miaka minne na hukumu kutolewa katika mazingira tatanishi kama
ilivyokuwa kwangu, Watanzania wa kawaida wanateseka kiasi gani?” alihoji
Mbowe.
Alidai kuwa baada ya kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja au faini ya Sh1,000,000, Hakimu Denis Mpelembwa amepandishwa cheo kuwa hakimu mkazi na kuhamishiwa mkoani Kagera, siku moja tu baada ya hukumu.
“Kilichokuwa kinatafutwa ni namna ya kumzuia Mbowe asigombee ubunge Hai kwa sababu CCM wanajua nguvu yangu. Wamekosea sana kwa sababu hukumu ile hainizuii kugombea. Nitaombea na nitashinda kwa kishindo,” alisema.
“Ninao wanasheria mahiri ambao baada ya kupitia hukumu yangu kwa harakaharaka, wamenihakikishia kwamba adhabu ile hainizuii kugombea na wanaendelea na taratibu nyingine za kisheria kuiomba Mahakama Kuu kuitangaza kuwa batili,” alisema.
Atoa gari la taka
Katika tukio jingine, mbunge huyo alikabidhi gari na mtambo wa kukusanya na kusindika taka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hai wenye thamani ya zaidi ya Sh200 milioni.
“Gari hili nimelinunua kwa fedha zangu na kulipa gharama zote na ushuru baada ya Serikali kuniwekea mizengwe. Nalikabidhi kwa halmashauri kusaidia kuzoa taka ili kuweka jimbo letu katika hali ya usafi kama ilivyo kwa Manispaa ya Moshi,” alisema Mbowe.
Wabunge wanena
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wabunge waliohudhuria mkutano huo, Pauline Gekul, Grace Kiwelu, Rose Kamili na Joseph Selasini waliwaomba wakazi wa Hai kuhakikisha Mbowe anarejea tena bungeni kutokana na uwezo wake wa kiuongozi.
“Ili tufanikishe lengo la kumrejesha Mbowe bungeni na wagombea wengine wa Chadema, mnatakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kujitokeza kupiga na kulinda kura Oktoba 25, mwaka huu,” alisema Gekul.

No comments:
Post a Comment