Waziri
mkuu wa zamani Mh. Edward Lowasa ameendelea na ziara yake ya kutafuta
wadhamini katika mikoa ya Katavi na Rukwa na kupata maefu ya wadhamini
na amewataka waananchi waliojiandikisha kutunza vizuri shahada zao
kwani ndio tiketi ya kuwawezesha kufikia ndoto zao za kuchagua kiongozi
wanayemtaka.
Mh.
Lowasa baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mpanda na kupata
mapokezi kishindo na wadhamini zaidi ya elfu tatu aliwashukuru wote
waliompokea na kuwataka kuendelea kuhamasishana kujiandikisha na
baadaye kupiga kura muda ukifika.
Awali
mwenyekiri wa CCM wa mkoa wa Katavi Bw Mselem Saidi Abdllah aliwataka
wanaccm kote nchini kuwatendea haki wagombea wote wanaotafuta wadhamini
kwani kwa vyovyote vile mmoja wao ndiye atakayekuwa kiongozi wao.
Lowasa
ambaye pia jana alitembelea mkoa wa Rukwa na kupata wadhamini wengi,
leo ataendelea kutafuta wadhamini katika mkoa wa Kagera.
No comments:
Post a Comment